Mgeni Rasmi Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (wa tatu kushoto) pamoja na wageni wengine waliohudhuria Sherehe hizo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Uchumi, Jeshi la Kujenga Taifa Kanali Felix Samilani, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Raphael M. Muhuga, Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhe. John Henjewele, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara, na Mkuu wa Kiteule cha Bulamba Meja David Msakulo.
Mgeni Rasmi Waziri wa Maendeleao ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (MB) akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mradi wa Ufugaji wa Samaki ndani ya Ziwa Viktoria Kiteule cha Bulamba kwa kutumia teknolojia mpya ya vizimba (Cages). Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhe.John Henjewele, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael M. Muhuga.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani akipandikiza vifaranga vya samaki ndani ya Ziwa Victoria, mradi unaotekelezwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Wilaya ya Bunda, Kiteule cha Bulamba kwa kutumia teknolojia mpya hapa nchini ya kuzalisha samaki kwenye vizimba.







No comments:
Post a Comment