Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 19 November 2014

KOREA KASKAZINI HATARINI KUFIKISHWA ICC

Viongozi wa Korea Kaskazini
Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu limesema Korea Kaskazini inastahili kufikishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kutokana na kukiuka haki za binadamu.

Katika baraza hilo zimetolewa tuhuma dhidi ya Korea Kaskazini kwamba serikali yake imekuwa ikifanya vitendo vya ukiukaji haki za binadamu.
Mapendekezo hayo yaliyopitishwa na baraza la haki za binadamu la kimataifa yanapaswa kupigiwa kura ili kupitishwa na bunge yaweze kuhalalishwa.
Ripoti ya mwezi Februari mwaka huu iliyotolewa na umoja wa mataifa ilibainisha kuwa watu wa Kawaida Korea Kaskazini wanakabiliawa na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu na pia mauaji.
Umoja wa mataifa unafanya uchunguzi dhidi ya Korea Kaskazini ili kupata ushahidi wa majina ambayo yapo kwamba taifa hilo limeua, likitesa watu,ukatili wa kisiasa na uhalifu mwingine.
Hata hivyo China na Urusi wanaoshikilia kura ya Veto katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,wamepingana na mapendekezo hayo ya Baraza la Usalama, huku nayo Korea Kaskazini ikiipinga ripoti hiyo.
Wanadiplomasia wana wasiwasi kuwa huenda China inataka kutumia kura yake ya Veto kupinga Baraza la Usalama kupeleka kesi zake katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC.
CREDIT: BBC/SWAHILI

No comments:

Post a Comment