Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 17 November 2014

DK. SLAA APOKEA KIJITI 'OPERESHENI DELETE CCM'

Dk. Slaa apokea kijiti Oparesheni Delete CCM
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Taifa, Freeman Mbowe, amehitimisha ngwe yake ya ziara ya Operesheni ‘Delete’ CCM, akikabidhi kijiti kwa Katibu Mkuu Dk. Willibrod Slaa, huku akiendelea kusisitiza kuwa salama ya nchi kuepukana na anguko kubwa ni chama kilichoko madarakani kuondoka.

Amesema kuwa, ufisadi unaoitikisa nchi kwa sasa wa IPTL kwenye Akaunti ya Escrow na ujenzi wa bomba la gesi, vitaiangusha Serikali ya CCM kama Rais Jakaya Kikwete hatamfukuza kazi Waziri Mkuu Mizengo Pinda na kuvunja Baraza la Mawaziri.
Akizungumza jana kwenye mkutano wa jioni mjini Morogoro ukiwa ni mkutano wake wa mwisho katika ziara hiyo aliyoianza Novemba 5 mwaka huu katika vijiji vya Wilaya ya Igunga, Mbowe alisema kuwa, ufisadi huo unaotikisa taifa na kuhujumu ustawi wa wananchi, ni matokeo ya mfumo mbovu wa serikali unaoelelewa na CCM.
“Ndugu wananchi wa Morogoro, leo nahitimisha ngwe ya kwanza ya mikutano niliyofanya katika mikoa minne kwenye ziara ambayo wananchi wa Nata kule Igunga waliipatia jina la Operesheni Delete CCM yaani ODC…nimeanzia Tabora nikaimaliza, nikaenda Katavi nikaimaliza, nikaenda Kigoma nikaimaliza, nikaingia Morogoro.
“Leo naishia hapa mjini, namkabidhi Katibu Mkuu Dk. Slaa ambaye kesho ataendelea vijiji vya majimbo yaliyosalia kwa mkoa huu, ataendelea Dodoma, Singida na Manyara. Tumedhamiria kui-delete CCM kabisa, maana mzunguko wangu huu kwa mara nyingine wananchi wamezidi kudhihirisha kuwa salama yetu ni kuiondoa CCM madarakani,” alisema Mbowe.
“Kwa kweli tumedhamiria wala hatutakuwa na mzaha…tena nguvu ya upinzani imeongezeka mno kupitia Ukawa. Taifa hili haliwezi kuwa salama kama CCM bado iko madarakani. Tumedhamiria kuanzia uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji…wananchi wote wenye nia njema na taifa hili, wote wanaochukia dhuluma, ufisadi na maovu yanayofanywa na CCM.
“Tunataka kuunganisha nguvu ya Watanzania wote wa kila rika, wa jinsia zote, wa makabila yote, wa dini zote kuinusuru nchi yetu katika anguko kubwa linalosababishwa na ufisadi unaoatamiwa na CCM kupitia mfumo mbovu wa utawala wanaoulea…mnasikia yanayoendelea kuhusu ufisadi wa IPTL kwenye eneo moja tu la Akaunti ya Escrow.
“Kama hiyo haitoshi jamaa mliowaamini mkawapatia dhamana ya kuongoza wamepiga ‘dili’ nyingine…yaani hiyo ya IPTL ambazo ni bilioni 400 na ushee wameona haitoshi, wamepiga tena trilioni 1.40 kwenye ujenzi wa bomba la gesi…huu wa ujenzi wa gesi ni ufisadi uliovunja rekodi ya kashfa zote kufanywa na serikali ya CCM dhidi ya wananchi wake,” alisema Mbowe na kuongeza.
“Salama ya nchi yetu kwa sasa ni kuiondoa CCM madarakani…lakini kwa muda huu kama Rais Kikwete hataki kuona aibu nyingine ya serikali yake kuvunjika ni yeye kumfukuza kazi Waziri Mkuu Pinda na kuunda upya Baraza la Mawaziri. Hili la sasa limeshindwa, Waziri Mkuu ameshindwa.
“Ufisadi wa IPTL na huo wa gesi wakubwa wamehusika…Ofisi ya Waziri Mkuu imekatiwa sehemu ya mabilioni hayo, akina Profesa Tibaijuka wamekatiwa, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu imekatiwa, Ikulu inajua, familia ya Rais inajua dili nzima ilivyofanyika…hawana pa kutokea tena serikali hii.”
Akizungumzia kuhusu Ukawa, Mbowe aliema kuwa umoja huo ni matokeo ya kilio cha wananchi cha muda mrefu kutaka kuunganisha nguvu ya wapinzani wa kweli kukiondoa CCM ambacho kimekuwa madarakani kwa zaidi ya nusu karne sasa.
Alisema kuwa, wapo watu ambao wameanza kuibua hoja za propaganda dhidi ya umoja huo wakisema kuwa viongozi wa juu hawataelewana kwa sababu ya kugombea urais, ambako alibainisha hawakuungana kwa ajili ya kugawana vyeo bali kujenga upinzani imara kwa ajili ya kuwakomboa wananchi kutokana na mikakati na sera za CCM kushindwa.
CREDIT: TANZANIA DAIMA

No comments:

Post a Comment