Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 1 November 2014

DIWANI ATOA MSAADA SHULE YA MSINGI ENGIRA


Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny Blog

Arusha: DIWANI wa kata ya Themi jijini Arusha, Milance Kinabo amewataka wadau wa elimu hapa nchini kuhakikisha wanazisaidia shule za kata kutatua kero mbalimbali zinazozikabili na kuacha kuiachia serikali pekee, hatua ambayo itasaidia kuinua kiwango cha elimu na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wanaosoma katika shule hizo.

 Kinabo alitoa rai hiyo mwishoni mwa wiki katika shule ya msingi Engira iliyopo jijini hapa, wakati akikabidhi vifaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya shule zikiwemo ndoo za  kuchotea  maji ,kufuatia uongozi wa shule hiyo kumweleza diwani huyo juu ya changamoto zinazoikabili shule hiyo .
 Alisema ipo haja kwa jamii ,taasisi na makampuni mbalimbali kwa ujumla wao kuona umuhimu  wa kujitoa kwa kuchangia elimu katika shule za kata ambazo baadhi yake zinakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vifaa vya kufundishia na madawati.
‘’leo nimekabidhi vifaa kwa ajili ya matumizi ya chooni pamoja na ndoo za maji zitakazo wasaidia wanafunzi wanapokuwa wanatumia vyoo kutokana na kutokuwepo miundo mbinu ya maji katika vyoo hivyo ni vizuri jamii pia ikaona umuhimu wa kuzisaidia shule hizi kwani serikali ina mambo  mengi,’’ alisema Kinabo.
Aidha diwani huyo ameahidi kusaidia bila kutegemea wafadhili shule zote za msingi zilizopo katika kata hiyo na kuondoa changamoto zinazozikabili,huku akitoa wito kwa wazazi kuhakikisha wanawahimiza watoto wao kwenda shule.
 Kinabo alimhakikishia mwalimu mkuu wa shule hiyo,Simon Siara, wakati akimkabidhi vifaa hivyo kwamba hata kubali shule yeyote katika kata yake ikabiliwe na changamoto itakayosababisha wanafunzi kukwama kimasomo,ambapo aliahidi kutumia hata rasilimali zake kumaliza kero yoyote inayohusu wanafunzi.
 ‘’mimi ni mwanasiasa ila sifanyi hivi kwa lengo la kujipatia umaarufu,ispokuwa najaribu kuisaidia serikali kupunguza kero za msingi ili watoto wapate ufaulu mzuri na si vinginevyo,’ alisema Kinabo.
Diwani huyo aliahidi kuendelea kutatua kero zinazoikabili shule hiyo pamoja na shule zingine zilizopo katika kata hiyo ikiwemo ya kuchangia  gharama za malipo ya umeme na maji  pamoja na mishahara ya wlinzi wa shule,kero ambayo inasumbua shule nyingi jijini hapa.
 Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo,Simon Siara pamoja na kumpongeza diwani huyo kwa misaada yake ya mara kwa mara,alieleza changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo ikiwa ni pamoja kutokuwa na fedha kwa ajili ya malipo ya mlinzi wa shule ,mpishi na Ankara za maji.
 Pia shule hiyo haina  uzio wa shule unaosababisha wanafunzi kutoroka ama kuvamiwa na vibaka ambao mara nyingine hugeuza maficho katika eneo hilo,pamoja na wa kutokuwa na mwamko wa kuchangia maendeleo ya shule.

No comments:

Post a Comment