Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 5 November 2014

BUNGE LAIGEUKA KAMATI YA ZITTO

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC),Zitto Kabwe. PICHA|MAKTABA 
Na Boniface Meena, Mwananchi
Dodoma. Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah amesema Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), chini ya Zitto Kabwe haikufuata utaratibu ilipoagiza Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Michael Mwanda na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, James Andilile wakamatwe na polisi kwa kushindwa kuwasilisha mikataba 26 ya gesi na mapitio yake mbele ya kamati hiyo tangu mwaka 2012.
Juzi, viongozi hao wa TPDC walikamatwa na kupandishwa katika gari dogo la wazi (pick-up) la polisi na kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi ambako taarifa iliyotolewa baadaye jioni na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ilisema viongozi hao wameachiwa huru kusubiri sheria na taratibu za Bunge.
Kamanda Kova alisema baada ya kuwakamata, ilibainika kwamba katika Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge Sura ya 296; Kifungu cha 12 (3) kinamtaka Mwenyekiti wa PAC kupendekeza kwa Spika wa Bunge kwanza kuhusu jambo lolote aliloliona kama ni kosa.
Dk Kashililah alisema jana kuwa utaratibu haukufuatwa kwa kuwa Kamati ilitakiwa kumwandikia Spika wa Bunge kuhusu suala hilo ili aweze kutoa maelekezo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) ambaye ndiye angeshauri utaratibu gani ufanyike.
“Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge haikufuatwa, walimwandikia Spika lakini hakuwapo, hivyo hawakujibiwa kwani Spika angetoa maelekezo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Kutokana na kutokufuatwa huko kwa taratibu, ndiyo maana polisi waliwaachia,” alisema Dk Kashililah.
Kauli ya Dk Kashililah inatofautiana na ile ya Zitto aliyotoa juzi akisema: “Kamati imetumia mamlaka yake ya kulazimisha maagizo yake kutekelezwa na pale ambapo maofisa wa Serikali wanashindwa kutekeleza, PAC ina mamlaka ya kuchukua hatua za kisheria kama ilivyofanya.
“Tumewapeleka polisi maofisa wa umma wanaoshindwa kutekeleza maagizo ya Bunge kwa mujibu wa Sheria ya Kinga na Madaraka ya Bunge Kifungu cha 12 cha Sheria Namba 3 ya mwaka 1988.”
Alisema PAC iliomba mikataba hiyo kwa sababu kwa muda mrefu, kumekuwa na kilio cha Watanzania juu ya usiri wa mikataba. “Bunge au kamati zake zina mamlaka ya kufahamu mikataba ya Serikali kwa masilahi ya wananchi.”
Awali, wakati wa maswali na majibu jana, Naibu Spika, Job Ndugai alisema ni muhimu kamati zikaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuwa Ofisi ya Bunge ipo nyuma yao lakini akaeleza linapofikia jambo linalohusu Haki, Kinga na Taratibu ni muhimu Bunge likaheshimiwa.
Mvutano ulipoanzia
Mvutano kati ya PAC na vigogo hao ulianza Jumatatu iliyopita, baada ya kutimuliwa katika kamati hiyo kwa kushindwa kuwasilisha mikataba hiyo na kutakiwa kufanya hivyo baada ya siku mbili na baadaye kuongezewa hadi tano, bila mafanikio.
Katika utetezi walioutoa wiki iliyopita, viongozi hao walisema kwa mujibu wa taratibu, mikataba hiyo inatakiwa kupitia Ofisi za Bunge na si katika kamati.
Juzi, waliieleza kamati hiyo kwamba wameshindwa kuiwasilisha kwani kwa nyakati tofauti, wamewasiliana na Wizara ya Nishati na Madini na AG, Frederick Werema na kujibiwa kuwa mikataba hiyo haitakiwi kuonyeshwa hadharani.
Walisema kwa mujibu wa maelezo ya AG, mikataba hiyo ikiwekwa wazi, inaweza kuifanya Serikali ifunguliwe kesi na wawekezaji.
Awali, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga alisema kumekuwa na mwingiliano wa kamati za Bunge, kati ya PAC na Kamati ya Nishati na Madini na kuliomba Bunge iliangalie hilo.
Kitwanga alikuwa akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa Mbozi Magharibi (Chadema), David Silinde aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani kuhusu mikataba mikubwa ya gesi na mafuta ambayo ina manufaa kwa wananchi lakini TPDC imeshindwa kuiwasilisha kwenye kamati. Alisema PAC kazi yake ni kukagua hesabu na kamati ya nishati na madini ni utendaji, hivyo hawezi kujibu swali la Silinde kwa kuwa Ofisi ya Spika ndiyo inayoweza kutoa ufafanuzi huo na kisha wabunge wenyewe wataamua.
Hata hivyo, Mbunge wa Nzega, Dk Hamisi Kigwangalla aliomba mwongozo kwa Spika kutaka Kitwanga afute kauli yake kwamba kamati hazijui mipaka yake kwa kuwa inaweza kuleta shida wakati zitakapokuwa zinatoa maelekezo.
Ndugai alisema mpaka sasa hakuna taarifa ya migongano kwenye kamati isipokuwa misuguano midogomidogo.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment