Pages

Pages

Pages

Sunday 19 October 2014

WAMAREKANI WATOA MSAADA WA VIFAA VYA SHULE VYENYE THAMANI YA 10MIL/=


Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny Blog 
Arusha: SHIRIKA la Opportunity Education lenye makao makuu nchini Marekani limetoa msaada wa vifaa vya masomo mbalimbali kwa shule ya msingi na awali ya Michael vyenye thamani ya shilingi 10 milioni kwa malengo ya kuimarisha elimu hapa nchini.


Hataivyo vifaa hivyo ni vya masomo ya hisabati, maarifa ya jamii,kingereza,Stadi za kazi,ambapo vifaa hivyo vitaweza kuwasaidia wanafunzi kujifunza na kufanya majaribio mbalimbali.

Akiongea na wazazipamoja na walezi katika maafali ya nne ya darasa la saba katika shule hiyo mkuu wa shule hiyo Robart Karuga alisema kuwa vifaa hivyo walivipokea mwaka huu kutoka kwa wafadhili hao

Alidai kuwa vifaa hivyo ambavyo pia kati yake kuna mitaala ya kufundishia kutoka Marekani vimeweza kuwasaidia sana watoto kujifunza kwa umakini zaidi kama inavyofanya nchi ya Marekani na kutokana na hilo ufaulu nao umeongezeka kwa kiwango kikubwa.

Pia alisema,mpaka sasa wanafunzi wameshaonesha hata moyo wa kupenda na kuthamini sana shule kwa kuwa wana vifaa lakini pia kile ambacho wanajifunza huwa wanakiona sasa kwa hali hiyo imechangia sana kuweza kuona hata vipaji vya watoto.

“yaani ni kwamba kupitia huu msaada wa vifaa vya kufundishia tunachokifanya hapa ni kwamba tunachukua mtaala wa hapa nchini na ule marekani kisha tunafundishia yote sasa kwa hali hiyo kwanini watoto wasipende masomo haya hasa ya Sayansi’aliongeza  Karuga.

Katika hatua nyingine nao wahitimu hao wa darasa la saba walisema kuwa kinachosababisha watoto wa kike wasiweze kufanya vizuri katika masomo ya sayansi ni kutokana na mila potofu na ambazo ziomepitwa na wakati kuwa masomo hayo ni maalumu pekee kwa ajili ya watoto wa kiume.

Wanafunzi hao walidai kuwa utaratibu huo unachangia sana kuwaaangusha lakini pia kuwakatisha tamaa wanafunzi wa kike hasa wale ambao wanapenda masomo hayo ingawaje Serikali imeweka mikakati ya kuongeza  idadi ya wana sayansi wa kike.

January Munishi, mgeni rasmi katika mahafali hayo, alisema kuwa upo uwezekano tena mkubwa san kwa wanafuzni kufanya vema mashuleni na hili hilo liweze kutokea kunahitajika umoja baina ya wazazi,walezi ambapo kwa kufanya hivyo kutaweza kuruhusu mafanikio katika safari ya elimu kwa wanafunzi.

No comments:

Post a Comment