Pages

Pages

Pages

Sunday 19 October 2014

DAWA YA WATOTO WA MITAANI YATAJWA

Chakula kikitolewa shuleni hupunguza wimbi la utoro unaosababisha kuwepo kwa watoto wa mitaani.

Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny Blog
Arusha: SHULE  za msingi zimeshauriwa kuungana kwa pamoja katika kuanzisha mpango maalum wa kuwasomesha na kuwsaidia  watoto yatima na wenye uhitaji ili kupunguza ongezeko  la watoto wa mitaani ambalo limekuwa likiongezeka siku hadi siku.


Ushauri huo ulitolewa  na mkurugenzi wa shule ya awali na msingi ya Mekson, Mecky Shirima, alipokuwa akizungumza na walezi na wadau wa elimu katika mahafali ya tatu ya darasa la saba ya shule hiyo ambapo jumla ya wanafunzi 34 walitunukiwa vyeti vya kumaliza darasa la saba.

Shirima alisema kuwa watoto yatima na wenye uhitaji wamekuwa wakikosa elimu na huduma nyinginezo za msingi lakini endapo shule zote za msingi zitaungana kwa pamoja kuwasomesha watoto hao ni wazi kuwa hapatakuwepo tena tatizo hilo.

Alisema kuwa ongezeko hilo la watoto wa mitaani linatokana na watoto hao kukosa malezi bora ya elimu na kwamba endapo kutakuwepo na mpango huo utasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza tatizo la watoto wa mitaani.

Alifafanua kuwa katika kuhakikisha kuwa watoto yatima na wenye uhitaji  wanapata elimu sawa na wengine shule hiyo imeweza kuwasomesha  bure watoto kumi  huku ikiwa imejiwekea mpango maalum wa kuwasaidia watoto walemavu wanaotokea katika familia duni.

“Wakurugenzi wa hizi shule za msingi wanapaswa kuangalia namna ya kuwasaidia hawa watoto wenye uhitaji kwani nao wana haki ya kupata elimu sawa na wengine sasa wasiposaidiwa hivi hili tatizo watoto wa mitaani litaisha kweli au ndio litazidi kuongezeka," aliongeza Shirima.

Nae meneja wa shule hiyo Ernester Shirima alisema kuwa shule hiyo imejizatiti katika kusaidia watoto wanaotokea katika familia duni lakini bado inakabilwa na changamoto ya wazazi kutofuatilia maendeleo ya watoto wao jambo ambalo linawakatisha tama walimu.

Alitaja changamoto ingine inayoikabili shule hiyo kuwa ni pamoja na wazazi kutolipa ada kwa wakati na hivyo kuifanya shule ishindwe kujiendesha yenyewe na hivyo kuwataka wazazi na walezi kushirikiana ili kuhakikisha kuwa shule inaweza kutimiza malengo yake ya kutoa elimu bora.

No comments:

Post a Comment