Pages

Pages

Pages

Sunday 19 October 2014

MILIONI 170/= KUWASAIDIA WANAWAKE NA VIJANA MERU KILA MWEZI


Na Mwandishi Wetu, Brother Danny Blog
Arusha: HALMASHAURI ya Meru iliyopo mkoani hapa imetenga kiasi cha shilingi milioni 170 kwa kila mwezi kwa kipindi cha Julai 2014 hadi Juni 2015 kwa ajili ya kuwasaidia wanawake na vijana kuendesha vikundi vya kuwafanya waondokane na umasikini.


Aidha fedha hizo zitatokana na mapato ambayo yatakuwa yanakusanywa na halmashauri hiyo kwa kila mwezi na hivyo kuwafanya wanawake kuweza kujiendeshea miradi yao.

Hayo yalisemwa na  makamu mwenyekiti wa halamsahuri hiyo Frida Kaaya alipokuwa akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani mara baada ya kutetea kiti chake baada ya kufanyika uchaguzi wa makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo.

Frida alisema kuwa kwa kipindi amabcho yupo kwenye kiti hicho ametetea nafasi ya wanawake katika kuhakikisha kuwa wanapata asilimia kumi ya mapato ya kila mwezi ya halimashauri hiyo ili ziweze kuwasaidia katika miradi yao.

“mimi nahidi ushirkiano kuwatetea wanawake wenzangu pamoja na kutetea miradi ya wananchi ili kuweza kuharakisha maendeleo kwa wananchi wetu na zaidi wanawake lazima wanufaike na fedha za halmashauri ili waweze kujikimu katika maisha yao kwa kuendeleza vikundi vya kuweka na kuopa”alisema makamu

Aliongeza kuwa fedha hizo zitaweza kuwanufaisha wanawake wa kata zote 17 ambazo zipo katika halimashauri hiyo ambapo kila kata ina jumla ya vikundi 10 vya kuweka na kukopa ambavyo tayari vimeshasajiliwa
kisheria.

Aidha alitaja changamoto zinazowakabili wanawake wa halmashauri hiyo kuwa ni pamoja na kutokuwa na mitaji ya kutosha kwa kuwa bado wengi wao hawana vigezo vya kutosha vya kukopa katika mabenki.

“hapa meru tumejitahidi kuwasaidia wanawake ili waweze kupata fursa za kukopa katika mabenki ambapo tumefanikiwa kuwaunganisha katika benki ya meru community ambapo kupitia benki hii ndio tu wanweza kukopa ili waweze kukidhi malengo ya mitaji yao na hivyo kuweza kuondokana na umasikini”aliongeza.

No comments:

Post a Comment