Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 21 October 2014

WACHEZAJI WA ARUSHA WALIOKWENDA BRAZIL WANUSURIKA KUADHIRIKA




Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny Blog
Arusha: VIJANA  wanaounda timu ya wachezaji wa mpira wa miguu ya  The Dream Team, ya Usa River, wilayani Arumeru,  iliyokwenda nchini Brazil kwenye Kombe la Dunia wameponea chupuchupu kuadhirika kwenya fainali ya Kombe la Nyerere Day, baada ya kulazimishwa sare ya bila kwa bila na timu ya African Amin Academy, na kulazimika kushinda kwa  penati.

The Dream team,  iliyocheza na wachezaji pungufu baada ya mchezaji mmoja kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 33, kipindi cha kwanza baada ya kumpiga kiwiko golikipa wa timu ya African Amin Academy, ya Ngarenanyuki, wilayani Arumeru, kwenye  fainali ya mashindano hayo yaliyofanyika kwenye uwanja wa Ngaresero, mji mdogo wa  Usa River.
Alikuwa ni mchezaji Edward Mpanda, ambae ni miongoni mwa vijana walioenda nchini Brazil, kwenye Kombe la Dunia kutumia ufundi kupiga penati ya mwisho iliyoipa  ushindi timu hiyo ya The Dream team na hivyo kuibuka kwa ushindi wa magoli 5 kwa 4.
Timu hizo zililazimika kupigiana matuta baada ya kumaliza dakika 90 bila ya kufungana ambapo katika hatua ya matuta ndipo timu hiyo inayoundwa na wachezaji walioenda Brazil, kuibuka kidedea baada ya kupata penati zote tano huku timu ya African Amin Academy ya Ngarenanyuki,ikipata penati 4 na kukosa moja iliyopanguliwa na golikipa wa The Dream Team.
Timu hizo zikichaza mbele ya mgeni rasmi aliyeandaa mashindano hayo, Kenedy Mpumilwa, na kushuhudiwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru, Nyerembe Mnasa, ambaye ndiye mlezi wa timu hiyo ya The Dream, ambapo alikuwa na wakati mgumu na kushindwa kutulia kwenye meza ya mgeni rasmi akionyesha wasi wasi wa timu yake kama ingeliibuka na ushindi.
Hali hiyo ilitokana na timu zote kucheza mpira wenye ufundi wa hali ya juu ambapo hata hivyo ilionekana timu ya Brazil ikifunikwa na vijana hao wa African Amin  ambao walicheza soka la kiwango cha juu na kuvutia  na kusababisha mashabiki kuwashangilia kila mara.
Katika mchezo huo washindi walipewa kikombe na fedha taslim,ambazo walikabidhiwa na mgeni rasmi Kenedy Mpumilwa, ambae ndie aliyeaandaa mashindano hayo yenye lengo la kumuenzi Mwalimu Nyerere.
Awali timu ya wasichana ya Testmony ya jijini Arusha, iliifumua bila huruma timu ya The Dream timu ya Usa River wilayani Arumeru kwa magoli 4-0 na kutwaa ubingwa wa kombe la kumbu kumbu ya miaka 15 ya kifo cha Mwalimu Nyerere.
Katika mchezo huo timu ya Testmony, ilitawala vipindi vyote vya mchezo huo na mpira kuchezwa nusu uwanja na kuifundisha timu hiyo ya The Dream Team, namna mpira wa miguu unavyochezwa na kufanikiwa kupata ushindi huo mnono.
Wakicheza kwa kasi na kwa ufundi wa hali ya juu iliwachukua Testmony, dakika 15 kujipatia goli la kuongoza lililofungwa na Asia Mohamed, baada ya kuwalamba chenga walinzi wa The Dream Team.
Goli la pili lilifungwa dakika ya 25  baada ya walinzi wa The Dream team, kujifunga katika harakati za kuokoa kutokana na shambulizi la nguvu lililoelekezwa langoni mwao ,Dakika ya  19 kipindi cha pili timu ya Testmony ilifanya shambulizi lingine la nguvu ambapo walinzi wa Dream, wakiwa katika harakati za kuokoa walijifunga  na goli la nne lilifungwa dakika ya 25 kipindi cha pili na Rukia Hussein baada ya kuwalamba chenga walinzi wa Dream team.
Kocha msaidizi wa timu ya Testmony Dikson Saidi siri ya mafaniko ya timu hiyo ilikuwa ni kujiandaa na kutoa onyo kwa timu watakazo kutana nazo kwenye mashindano mbalimbali kukutana na kipigo kama hicho,mchezo huo ulichezeshwa na Mwamuzi Joseph Mandawa kutoka Arusha.

No comments:

Post a Comment