Pages

Pages

Pages

Tuesday 12 August 2014

KWA WADADA: UNATAKA TUMBO LAKO LIWE FLAT? FANYA HIVI - 8


Leo ni siku ya nane ya mazoezi ya siku 21 ya kupunguza unene wa tumbo. Nitawaambia kitu kimoja akinadada mnaohangaika kupunguza unene wa matumbo na mnataka matumbo yenu yawe flat. Wapo wengi wanaohangaika kutafuta dawa za kuondoa mafuta mwili. Msifanye hivyo, mtapata kemikali nyingine za sumu ambazo zitakuwa na madhara kwenye afya zenu.
Wengine wanajinyima kula na kujishindisha njaa; angalieni msije mpakata vidonda vya tumbo bure mkaongeza matatizo mengine.
Mbinu hapa ni moja tu: mazoezi ya mpangilio pamoja na vyakula visivyokuwa na mafuta ambavyo haviongezi unene!
Siku ya leo unapaswa kufanya mazoezi kwa dakika 45 mfululizo.

Tumia mashine za mazoezi (Treadmill)
Tumia mashine maalum za mazoezi, ambazo zinapatikana kwenye gym au kama una uwezo unaweza kuinunua mwenyewe. Uiseti katika asilimia moja ili kuepuka kuteleza, lakini unaweza kuongeza kasi ama kuipunguza, kutegemeana na namna ulivyo fit. Kwa zoezi hili utapunguza mafuta mengi mwilini. Angalia mwongozo huu hapa chini, ambao unaweza kuuchapisha na kuubandika ukutani.

Juisi ya Parachichi


Ukishamaliza mazoezi na kupumzika, pata juisi murua ya parachichi ambayo inasaidia mmeng'enyo wa chakula.

No comments:

Post a Comment