Pages

Pages

Pages

Tuesday 12 August 2014

MWANAHABARI FULGENCE MALANGALILA AFARIKI DUNIA

Mzee Fulgence Malangalila (kulia) akipokea picha ya Daudi Mwangosi kutoka kwa Mwenyekiti wa IPC, Frank Leonard, baada ya maandamano ya wanahabari mkoani Iringa kukumbuka miaka miwili ya kifo cha Mwangosi.

Mmoja wa waasisi wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Iringa (IPC), Mzee Fulgence Malangalila, amefariki leo hii mjini Iringa.
Katibu Mtendaji wa IPC, Francis Godwin, amethibitisha kutokea kwa msiba huo na kwamba mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwa marehemu Frelimo katika Manispaa ya Iringa.
Kwa mujibu wa Bw. Godwin, marehemu alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kisukari na mauti yamemfika akiwa amelazwa kwenye Hospitali ya Mkoa wa Iringa alikolazwa kwa takriban siku nne zilizopita.
Enzi ya uhai wake, marehemu aliwahi kuandikia vyombo mbalimbali vya habari, hasa magazeti - yakiwemo ya kampuni ya Business Times, lakini pia amepata kuandika vitabu kadhaa.
Maziko yanatarajiwa kufanyika kesho.
MWANGA WA MILELE AKUANGAZIE EE BWANA ... UPUMZIKE KWA AMANI!

No comments:

Post a Comment