Dar es Salaam. Mwanachama wa Yanga na Mwenyekiti wa Ujenzi wa
Jengo la Mafia, Ridhiwani Kikwete amepinga kitendo cha Mwenyekiti wa
klabu hiyo, Yusuph Manji na wenzake kuongezewa muda wa uongozi wa mwaka
mmoja.
Ridhiwani aliyasema hayo katika mahojiano maalumu
na gazeti hili mjini Dodoma hivi karibuni na akaipinga wanachama wa
klabu hiyo kuuuongezea muda uongozi uliopo madarakani unaoongozwa na
Manji na kuwashauri wafanye uchaguzi kuwachagua tena na si kuwaongezea
muda wakati wameshamaliza kipindi chao kwani huo ni uvunjifu wa katiba.
“Klabu ya Yanga maendeleo yake mimi binafsi
hayaniridhishi kwa sababu kuna vitu vingi vinafanyika ndivyo sivyo. Kwa
mfano, mambo yanayotokea sasa ya migogoro ya kikatiba, kwamba watu
wanaamua tu kubadilisha katiba.
Wanachama wanakutana wanaamua kumwongezea muda
kiongozi, tena muda wenyewe bora wangeongeza awamu nzima, lakini
wanamwuongezea mwaka mmoja ili iweje?, Hhii si nzuri, sijapenda hata
kidogo.
“Kitu kimoja ninachojua ni kwamba , Yanga
wanatakiwa kufanya uchaguzi Julai, kwa maana kile kipindi chao
kimekwisha., Yanga ni klabu ambayo inaongozwa na taratibu kwa maana ya
kwamba watu wanatakiwa kufuata katiba yao,i,” alisema Ridhiwani.
Aliongeza: “Kwa nini tufikie sehemu ya kuchagua
kiongozi kwa mwaka mmoja?. Mimi nafikiri jambo la msingi wanalotakiwa
kufanya kama wao wanamtaka Yusuph (Manji) kama wanachama wamshawishi
Manji agombee na baada ya kugombea wamchague hiyo miaka minne yake,
halafu yeye aongoze mwaka wake mmoja na baada ya hapo aseme mimi
nimechoka ajiuzulu halafu hiyo miaka mitatu inayobakia aiache, hivyo
ndivyo inatakiwa kuwa.”
Ridhiwani alisema Yanga inaongozwa kisheria na
haiongozwi kwa uamuzi wa mtu binafsi wakati kuna katiba ambayo ndiyo
mwongozo wa klabu hiyo.
“Leo mtu anaamka anasema anataka niongoze mwaka
mmoja, lakini jambo jljingine linalonikwaza ni kusuasua kwa shughuli za
kimaendeleo., Sshughuli nyingi za kimaendeleo zimekuwa zinafanywa kwa
mazoea ya kawaida tu hakuna kufikiri na kutazama kesho Yanga
inaendeshwaje.
“Kwa mfano, Yanga kulikuwa na mpango wa kujenga
uwanja, watu wanang’ang’ania uwanja ujengwe Jangwani bila kujua pale ni
mjini, lakini pili eneo lenyewe liko wapi la kujenga uwanja, tatu, hata
hizo hati zenyewe zinazotakiwa zitumike katika kujenga uwanja hazipo
pale Yanga, zipo kwa mtu., Ssasa haya ni mambo ambayo hayanifurahishi.
“Nadhani viongozi inabidi wakajipange vizuri na
kuona ni namna gani wanaweza kutatua migogoro na wanachama., Hhata huyo
mzee ambaye ameshikilia hizo hati wamwite wazungumze naye aweke hati
zile ili mambo yaendelee kwani haya mambo ya ngoja ngoja hayawezi
kuisaidia Yanga,” alisema.
No comments:
Post a Comment