Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 18 July 2014

RIDHIWANI APINGA YUSSUF MANJI KUONGEZEWA MUDA YANGA


Mwenyekiti wa klabu ya Yanga iliyopo mtaa wa Jangwani, Yusuph Manji

Dar es Salaam. Mwanachama wa Yanga na Mwenyekiti wa Ujenzi wa Jengo la Mafia, Ridhiwani Kikwete amepinga kitendo cha Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuph Manji na wenzake kuongezewa muda wa uongozi wa mwaka mmoja.
Ridhiwani aliyasema hayo katika mahojiano maalumu na gazeti hili mjini Dodoma hivi karibuni na akaipinga wanachama wa klabu hiyo kuuuongezea muda uongozi uliopo madarakani unaoongozwa na Manji na kuwashauri wafanye uchaguzi kuwachagua tena na si kuwaongezea muda wakati wameshamaliza kipindi chao kwani huo ni uvunjifu wa katiba.
“Klabu ya Yanga maendeleo yake mimi binafsi hayaniridhishi kwa sababu kuna vitu vingi vinafanyika ndivyo sivyo. Kwa mfano, mambo yanayotokea sasa ya migogoro ya kikatiba, kwamba watu wanaamua tu kubadilisha katiba.
Wanachama wanakutana wanaamua kumwongezea muda kiongozi, tena muda wenyewe bora wangeongeza awamu nzima, lakini wanamwuongezea mwaka mmoja ili iweje?, Hhii si nzuri, sijapenda hata kidogo.
“Kitu kimoja ninachojua ni kwamba , Yanga wanatakiwa kufanya uchaguzi Julai, kwa maana kile kipindi chao kimekwisha., Yanga ni klabu ambayo inaongozwa na taratibu kwa maana ya kwamba watu wanatakiwa kufuata katiba yao,i,” alisema Ridhiwani.
Aliongeza: “Kwa nini tufikie sehemu ya kuchagua kiongozi kwa mwaka mmoja?. Mimi nafikiri jambo la msingi wanalotakiwa kufanya kama wao wanamtaka Yusuph (Manji) kama wanachama wamshawishi Manji agombee na baada ya kugombea wamchague hiyo miaka minne yake, halafu yeye aongoze mwaka wake mmoja na baada ya hapo aseme mimi nimechoka ajiuzulu halafu hiyo miaka mitatu inayobakia aiache, hivyo ndivyo inatakiwa kuwa.”
Ridhiwani alisema Yanga inaongozwa kisheria na haiongozwi kwa uamuzi wa mtu binafsi wakati kuna katiba ambayo ndiyo mwongozo wa klabu hiyo.
“Leo mtu anaamka anasema anataka niongoze mwaka mmoja, lakini jambo jljingine linalonikwaza ni kusuasua kwa shughuli za kimaendeleo., Sshughuli nyingi za kimaendeleo zimekuwa zinafanywa kwa mazoea ya kawaida tu hakuna kufikiri na kutazama kesho Yanga inaendeshwaje.
“Kwa mfano, Yanga kulikuwa na mpango wa kujenga uwanja, watu wanang’ang’ania uwanja ujengwe Jangwani bila kujua pale ni mjini, lakini pili eneo lenyewe liko wapi la kujenga uwanja, tatu, hata hizo hati zenyewe zinazotakiwa zitumike katika kujenga uwanja hazipo pale Yanga, zipo kwa mtu., Ssasa haya ni mambo ambayo hayanifurahishi.
“Nadhani viongozi inabidi wakajipange vizuri na kuona ni namna gani wanaweza kutatua migogoro na wanachama., Hhata huyo mzee ambaye ameshikilia hizo hati wamwite wazungumze naye aweke hati zile ili mambo yaendelee kwani haya mambo ya ngoja ngoja hayawezi kuisaidia Yanga,” alisema.
Pia, Ridhiwani alisema ujio wa kocha mpya, Marcio Maximo utasaidia kuboresha mpira wa timu hiyo, lakini akashauri uongozi kuhakikisha wanaanzisha programu za watoto ili kuwawekea misingi mizuri ya soka kwa maendeleo ya klabu.
CREDIT: MWANANCHI
       

No comments:

Post a Comment