Taarifa ya Mikutano ya Hadhara ya ACT
Ndugu wanachama wa ACT-Tanzania, wapenzi wa chama na watanzania wote kwa ujumla, tunawasalimu tena kwa salamu inayoashiria mabadiliko na uwazi.
Kama
tulivyokuwa tumeahidi wakati tunajibu swali la wadau kwamba ni kwa nini
hatufanyi mikutano ya hadhara; na tukafafanua kwamba Chama kilikuwa
kinajipanga tena kuanza mikutano ya hadhara, sasa mipango tuliyokuwa
tumewaahidi imekamilika na sasa tunatimiza!.
ACT-
Tanzania, tunapenda kuwataarifu kwamba chama kinatarajia kuanza kufanya
mikutano ya hadhara leo tarehe 19/ 07/2014 Mungu akipenda!. Ziara hiyo
inatarajiwa kufanyika katika mikoa mitano (kwa kuanzia) Ambayo ni
Tabora, Katavi Kigoma na Kisha Singida na Mwanza.
Katika
ziara hiyo, leo tarehe 19/07/2014, viongozi wa chama wanatarajia
kuongoza mkutano mkubwa mkoani Tabora , tarehe 20/07/2014, wanatarajia
kufanya mkutano wa hadhara mkoani Katavi na 22/07/2014, Wataongoza
mkutano wa hadhara mkoani Kigoma. Ratiba ya muendelezo wa mikutano hiyo
katika mikoa mingine itakuwa inatolewa kwa kadiri itakavyoonekana
inafaa.Kadhalika mikutano mingine itakuwa inaendelea kufanyika katika
mikoa na wilaya tofauti tofauti nchini ikiratibiwa na viongozi wa ngazi
husika kuanzia leo.
MALENGO YA ZIARA;
Malengo ya ziara ya viongozi wakuu wa ACT-Tanzania mikoani ni pamoja na,
1. Kukitangaza chama kwa wananchi,
2. Kufungua Ofisi za ACT-Tanzania katika Mikoa,
3. Kupokea wanachama wapya ambao wataamua kujiunga na ACT-Tanzania,
4. Kufanya mikutano ya ndani inayolenga kukijenga chama ,
5. Kueleza misimamo ya chama kuhusu mambo mazito ya Kitaifa.
2. Kufungua Ofisi za ACT-Tanzania katika Mikoa,
3. Kupokea wanachama wapya ambao wataamua kujiunga na ACT-Tanzania,
4. Kufanya mikutano ya ndani inayolenga kukijenga chama ,
5. Kueleza misimamo ya chama kuhusu mambo mazito ya Kitaifa.
Katika
Ziara hizo, viongozi watakaohusika ni pamoja na Mwenyekiti wa Chama wa
muda ndugu Kadawi Limbu, Katibu Mkuu wa Chama wa muda ndugu Samson
Mwigamba , Katibu wa mawasiliano na Uenezi wa ACT-Tanzania ndugu Mohamed
Massaga na viongozi wengine wa maeneo husika.
Tutumie
fursa hii kuwasihi kufika kwa wingi katika mikutano hiyo na wale wote
watakaoweza kufika katika mikutano hiyo, wafike na kalamu na karatasi
kwa ajili ya kuandika mambo muhimu.
Ikumbukwe kuwa ACT-Tanzania inapambana kuijenga Tanzania iliyo bora zaidi kwa ustawi wa watanzania wote leo na kesho.
ACT-Tanzania....... Taifa kwanza leo na kesho,
Mabadiliko na uwazi ...........Chukua Hatua.
Tuwasiliane acttanzania@gmail.com au acttanzania@yahoo.com
No comments:
Post a Comment