Pages

Pages

Pages

Sunday 20 July 2014

ACT-TANZANIA YAANDAA MIKUTANO MIKUBWA NCHINI

Taarifa ya Mikutano ya Hadhara ya ACT

Ndugu wanachama wa ACT-Tanzania, wapenzi wa chama na watanzania wote kwa ujumla, tunawasalimu tena kwa salamu inayoashiria mabadiliko na uwazi.
Kama tulivyokuwa tumeahidi wakati tunajibu swali la wadau kwamba ni kwa nini hatufanyi mikutano ya hadhara; na tukafafanua kwamba Chama kilikuwa kinajipanga tena kuanza mikutano ya hadhara, sasa mipango tuliyokuwa tumewaahidi imekamilika na sasa tunatimiza!.
ACT- Tanzania, tunapenda kuwataarifu kwamba chama kinatarajia kuanza kufanya mikutano ya hadhara leo tarehe 19/ 07/2014 Mungu akipenda!. Ziara hiyo inatarajiwa kufanyika katika mikoa mitano (kwa kuanzia) Ambayo ni Tabora, Katavi Kigoma na Kisha Singida na Mwanza.
Katika ziara hiyo, leo tarehe 19/07/2014, viongozi wa chama wanatarajia kuongoza mkutano mkubwa mkoani Tabora , tarehe 20/07/2014, wanatarajia kufanya mkutano wa hadhara mkoani Katavi na 22/07/2014, Wataongoza mkutano wa hadhara mkoani Kigoma. Ratiba ya muendelezo wa mikutano hiyo katika mikoa mingine itakuwa inatolewa kwa kadiri itakavyoonekana inafaa.Kadhalika mikutano mingine itakuwa inaendelea kufanyika katika mikoa na wilaya tofauti tofauti nchini ikiratibiwa na viongozi wa ngazi husika kuanzia leo.
MALENGO YA ZIARA;
Malengo ya ziara ya viongozi wakuu wa ACT-Tanzania mikoani ni pamoja na,
1. Kukitangaza chama kwa wananchi,
2. Kufungua Ofisi za ACT-Tanzania katika Mikoa,
3. Kupokea wanachama wapya ambao wataamua kujiunga na ACT-Tanzania,
4. Kufanya mikutano ya ndani inayolenga kukijenga chama ,
5. Kueleza misimamo ya chama kuhusu mambo mazito ya Kitaifa.
Katika Ziara hizo, viongozi watakaohusika ni pamoja na Mwenyekiti wa Chama wa muda ndugu Kadawi Limbu, Katibu Mkuu wa Chama wa muda ndugu Samson Mwigamba , Katibu wa mawasiliano na Uenezi wa ACT-Tanzania ndugu Mohamed Massaga na viongozi wengine wa maeneo husika.
Tutumie fursa hii kuwasihi kufika kwa wingi katika mikutano hiyo na wale wote watakaoweza kufika katika mikutano hiyo, wafike na kalamu na karatasi kwa ajili ya kuandika mambo muhimu.
Ikumbukwe kuwa ACT-Tanzania inapambana kuijenga Tanzania iliyo bora zaidi kwa ustawi wa watanzania wote leo na kesho.
ACT-Tanzania....... Taifa kwanza leo na kesho,
Mabadiliko na uwazi ...........Chukua Hatua.

No comments:

Post a Comment