Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Arusha
BAADHI ya Vijana wa Kanisa la KKKT Usharika wa Enaboishu Mtaa wa Chemchem Dayosisi ya Kaskazini Kati Mkoani Arusha wamelaani kitendo cha wanawake kuwatupa watoto wachanga pamoja na wanaochukua mikopo na kushindwa kurejesha Marejesho na baadaye kutelekeza familia baada ya kufilisiwa.
Akihubiri katika ibada ya kushuka kwa Roho Mtakatifu iliyoongozwa na Vijana kanisani hapo Mtumishi Godliving Godfrey ambaye ni mwenyekiti wa vijana alisema kuwa kitendo cha baadhi ya wanawake kuwatupa watoto kwenye mitaro ni jambo ambalo kanisa linapaswa kupiga vitana kutoa elimu juu ya madhara yanayoeweza kujitikeza kwa wale wanaoendekeza vitendo hivyo.
Akifafanua kwa upande wa mikopo,alisema kuwa kukopa fedha sio dhambi bali ni mbaya endapo mtu atachukua fedha za mikopo bila kuwa na shughuli maalum ya kufanyia fedha hizo ambapo aliwataka wazazi kushirikishana mawazo kabla ya kukopa fedha ili kuepuka kufilisiwa.
Alisema kuwa wapo baadhi ya wazazi ambao wanachukua fedha za mikopo bila kushirikishana jambo ambalo linazua ugomvi ndani ya familia na baadhi yao kutelekeza familia pindi taasisi ya kifedha au mtu anapofika kudai haki yake na kushindwa kumrejeshea.
Kwa upande wake Titos Augustino Mwimbaji wa nyimbo za injili ambaye alizindua albamu yake ijilikanayo kama MADHABAHU ZIMEPASUKA kanisani hapo alisema kuwa kitendo cha watoto kufungwa katika mifiko kisha kutupwa kwenye mitaro na wengine kufanyiwa ukatili wa kijinsia ni kinyume cha haki za binadamu.
Aliongeza kuwa ili matatizo hayo yaweze kuondoka ndani ya jamii ni jukumu la kila Mkristo kuomba kwa bidii ili Roho Mtakatifu aweze kuwashukia watu ambapo aliwaasa watumish kuongeza bidii kutoa elimu dhidi ya vitendo hivyo viovu ili jamii iweze kufahamu ni dhambi na haimpendezi Mungu.
Kwa upande wake Rabelson Lotha ambaye ni mwanafunzi katika shule ya Sekondari Enyoito Wilayani Arumeru Mkoani Arusha alisema kuwa zipo sababu nyingine zinazosababisha baadhi ya wazazi kutelekeza familia na wengine kuwatupa watoto kama vile ugumu wa maisha pamoja na ukosefu wa ushirikiano.
Hata hivyo walisema kuwa upo umuhimu wa wazazi kuwashirikisha watoto katika masuala ya maendeleo pamoja na familia kukaa pamoja pindi wanapo hitaji kuchukuwa fedha ili kuepusha migogoro wanaposhindwa kurejesha fedha za mikopo.
No comments:
Post a Comment