Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 12 June 2014

TBS BADO YAKABILIWA NA CHANGAMOTO LUKUKI


Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Arusha

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) bado linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo  uhaba wa wajasiliamali wachache kujitokeza kuthibitisha ubora wa bizaa zao na kuongeza thamani ya bizaa na kuweza kusambaza bidhaa zao ndani na nje ya nchi.
Hayo yalisemwa leo na Ofisa Uhusiano wa TBS, Bi.Roida Andusamile wakati wa maonyesho ya wiki moja  ya wajasiriamali yaliyodhaminiwa na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya makumbusho mkoani Arusha.
Hata hivyo alisema kuwa hali hiyo inasababisha wajasiliamali kutoweza kuiuuza kwa wingi biashara zao katika soko la ndani na nje ya nchi kutokana na kuwa na alama ya ubora wa viwango hali inayosababisha baadhi ya walaji kutonunua bizaa zao badala yake amewataka kujitokeza na kutumia fursa hiyo kwani usajili wa kupata hati ya ubora ni bure.
Aliongeza kuwa bado kumekuwepo na changamoto nyingine kwa wajasiliamali ya kuwepo kwa mazingira duni ya kuzalisha bizaa hali ambayo mazingira hayo hayaridhishi na kukidhi vigezo vya kupewa cheti cha ubora badala yake waboreshe mazingira ya uzalishji na kuweza kukidhi vigezo na kupewa cheti cha alama ya ubora.
Bi. Roida alisema kuwa niwajasiliamali 258 tu nchi nzima ambao wamejitokeza kupata cheti cha ubora ambapo idadi hiyo ni ndogo ukilinganisha wingi wa wajasiliamali nchini mbali na kuwapa elimu tangu mwaka 2005 karibu mikoa yote nchini lakini wamekuwa wakisuasua kuja kupata cheti hicho ambapo bizaa nyingi amabapzo hajijapata hati hiyo ni zachakula ikiwemo mango pickle,sabuni za maji na kipande na peanut butter, tomato sauce na bizaa nyinginezo.
Kwa upande wake mjasiamali bw,Ibrahimu Yahaya ambaye ni muuzaji wa viungo na mzalishaji achali alisema kuwa mbali na jitihada za kuweza kujiajili wenyewe ili kuweza kujikwamua iuchumi na kuondoa umaskini bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mitaji midogo ya kuweza kuendesha biashara zao sambamba na ukosefu wamasoko ya uhakika hali inayiowasababishia kutouza kwa wingi bizaa zao.
Aliongeza kuwa taasisi za kifedha kutoweza kuwakopesha kutokana na kuwa na masharti magumu ya kuwawezesha kupata mitaji na kuweza kupanua biashara zao nakuweza kupambana na adui umaskini kuanzia katika ngazi ya familia hadi taifa.

No comments:

Post a Comment