Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Thursday, 12 June 2014
DOLA MILIONI 1.5 ZATOLEWA KAMA MKOPO KWA WAFANYABIASHARA NA WAJASIRIAMALI
Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Arusha
JUMLA ya dola milioni 1.5 zimetolewa kwa mkopo katika kipindi cha miaka mitano na kampuni ya kukopesha mashine ya Equity for Tanzania (EFTA) kwa wajasiliamali wakulima na wafanyabiashara nchini, ili kuinua vipato vyao.
Akizungumza jana wakati wa uzinduzi wa tawi la kampuni hiyo, Jijini Arusha, Mkuu wa kampuni ya Equity for Tanzania (EFTA), Madeleine Anderson, alisema tangu waanze kutoa mikopo kwa wajasiliamali, jumla ya watu 120 wamenufaika kw akukopeshwa kiasi hicho cha fedha.
Alisema kuwa wao waliona bora waje na mfumno mpya wa kukopesha dhana,badala ya fedha, ili mtu asishindwe kufikia ndoto yake kwa kuwaza kurejesha au kuvuja fedha atakazopata.
"Sisi tunataka mtu aorodheshe tu vifaa vyake vya mashine anazotaka alafu tunampatia na tunaanz akutoa mkopo wa Shs. 16 hadi 80 milioni na dhamana ya mkopo hakuna, ila utarejesha kwa miaka mitatu," alisema.
Alisema tumepanga miaka mingi ili mteja aweze kuvuna faida kubwa na aweze kulipa bila shida, lakini pia ukirejesha mapema kabla ya miaka mitatu, unapatiwa bonus kulingana na muda wako uliowahisha kurejesha mkopo.
Madeleine alisema kutokana na kutoa huduma hiyo hawajapata changamoto kubwa, sababu wengfi wanajitahidi kurejesha kwa wakati na kumaliza mapema ili wengine waweze kukopa.
Naye mmoja wa wajasiriamali aliyekopa kwenye kampuni hiyo, Ally Dalos, alisema yeye alikopa mashine ya kutengeneza sabuni ya maji, mche na za kuongeza.
Alisema mkopo wa mshine yake uligharimu Shs.18.2, lakini kwa sababu ya kumlipa mapema, alifanikiwa kurejesha mkopo wake ndani ya miaka miwili kabla ya miaka mitatu kampuni wanayotaka na alipata bonus ya Shs. 500,000.
"Hii bonus ndiyo ilinisukuma nilipe mapema mkopo wangu bila kufuatwa fuatwa, hivyo naomba na wenzangu kampuni hii ndiyo njia ya kutokea kimaisha," alisema.
Kwa upande wa mjasiliamali mwingine, Godson Makundi, alisema yeye amenufaika na kampuni hiyo, kwa kukopa mashine za maabara ya thamani ya Shs. 24 milioni.
"Nilichukua mkopo huu Desemwa mwaka jana na januari nimeanza kazi na nimeanza kurejesha sababu inanilipa, hivyo watu wasiogope wachukue mikopo na sio kulalamikia serikali tu," alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment