Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 12 June 2014

WATUHUMIWA WA UGAIDI WATINGA KORTINI ARUSHA LEO



Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Arusha

Watuhumiwa  nane kati ya 16 waliopo katika kikundi cha kigaidi cha Al Shabab, jana wamepanda kizimbani kwa mara ya pili, kwa tuhuma za kujihusisha  kushawishi na kuhamasisha watu kujiunga na kikundi cha kigaidi cha Al Shabab.
Wahumumiwa hao ni Abdala Athumani, Swalehe Hamisi, Abdallah Yasini, Hassani Saidi, Sudi Lusuma,Abdulkarim Hasia na Shaban Wawa.
Aidha watuhumiwa hao waolikuwa mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Mustapher  Siyani na Wakili wa Serikali Helen Rwijage, waliomba Mahakama hiyo itoe amri ya kulitaka jeshi la polisi kuleta mahakamani simu,hati za kusafiria, nguo na viatu vyao, ili ndugu zao wakachukue mahakamani hapo ambako wanaamini mahali salama.
“Mheshimiwa hakimu tunaomba utoe amri Polisi walete vitu vyetu walivyotunyang’anya ambavyo anavyo, vije mahakamani ili viwe mahali salama na ndugu zetu wapewe,” walisema.
Wakati kesi hiyo ikiendelea  askari wa Magereza walilazimika kuzuia ndugu zao waliofika kwa wingi wakiwa wengi katika vazi la kanzu fupi za rangi nyeupe, kijivu na nyeusi mahakamani hapo, kushuhudia kesi hiyo, huku baadhi yao wakipekuliwa katika mikoba yao kama haina mabomu.
Pia waliomba mahakama hiyo itoe amri wapatiwe hati ya mashitaka yao, ndugu zao waruhusiwe kuwatembelea maabusu ili wapate haki zao za msingi kama vile sababu na vitu vingine.
“Mheshimiwa tunashangaa sisi haturuhusiwi kuonana na ndugu zetu na wakija wanazuiwa, sasa tunakosa sababu wala dawa ya mswaki, lakini pia matibabu hatupewi wakati tunaumwa, tukiongea hawatusikilizi,” walisema.
Hakimu Siyani alilazimika kumwita mmoja wa askari magereza atoe maelezo ya kuhusu kuzuiwa ndugu zao, ambapo naye alidai kuwa wapo katika hatua za mwisho za kuandaa utaratibu utakaofaa kuonana na ndugu zao, kulingana na mazingira ya kesi hiyo.
“Hata hivyo jamani mahakama hii haina mamlaka ya kusikiliza kesi hii, hivyo malalamiko yenu andikeni barua kwa mpelelezi wa kesi yenu orodhesheni madai yenu yote yeye ataoana kitu gani kinafaa mpewe au la kama kinahusika katika kesi, kama suala la simu endapo kuna ushahidi wa kuhusika na kesi haiwezekani mkapewa,”alisema.
Alitoa amri pia ya washitakiwa hao kupewa nakala ya hati ya mashitaka inayowakabili kila mmoja, sababu ni haki yao ya msingi. 

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 25 mwaka huu itakapotajwa tena.

No comments:

Post a Comment