Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Arusha
IKIWA leo ni Siku ya Mtoto wa Afrika baadhi ya watoto wa mitaani ambao hawana makazi maalumu katika jiji la Arusha wamewalaumu baadhi ya wazazi wasio waaminifu ambao wakati mwingine huwageuza kinyume cha maumbile na kisha kuwapa ujira wa kiasi cha shilingi mia tano.
Watoto hao walitoa kilio hicho mapema leo pembezoni mwa uwanja wa mpira wa sheikh amri abeid ambapo ndipo maskani yao wakati wakiongea na Brother Danny Blog kuhusiana na uhuru wao.Walidai kuwa watu wazima wakati wa usiku huwa wana warubuni tena watoto wa kiume kwa kuwadanganyana kisha kuwaaangilia kinyume cha maumbile na kisha kuwapa kiasi cha shilingi mia tano mpaka elfu moja.
Walisema kuwa kutokana na ugumu wa maisha wakati mwingine wanalazimika kufanya hivyo kwa kuwa hawana mahitaji muhimu ingawaje wanapata wakati mgumu wa maumivu.
No comments:
Post a Comment