Naam,
Siyo gari pekee linalowekwa kigogo (kizuizi kwenye gurudumu) linapokuwa kwenye limesimama kwenye mlima au mteremko, hata mkokoteni wa wanyamakazi kama huu nao unawekwa kizuizi.
Hapa punda wanaonekana wametulia baada ya 'dereva' wa mkokoteni huu kuweka kigogo kwenye gurudumu la kushoto na yeye kuingia mitaani.
Wenyewe wanasema, usipofanya hivyo hawa jamaa wanaondoka zao, na mzigo. Usiulize hapa ni wapi, ni ndani ya Tanzania, miaka 53 baada ya uhuru wa Tanganyika!
Kweli, akili ni nywele.

No comments:
Post a Comment