MAKAMU Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa ambaye pia ni Katibu wa PCT jijini Mwanza, Askofu Zenobius Isaya, anatarajia kuwaongoza Maaskofu na Wachungaji mbalimbali katika ufunguzi wa duka la Msama Promotions jijini Mwanza litakalofunguliwa Juni 17.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama Maaskofu hao sambamba na wachungaji wataweka wakfu kwa dua maalum itakayoongozwa na kiongozi huyo wa juu wa kiroho jijini humo.
Msama amesema shughuli za kuweka wakfu duka hilo linasindikizwa na shangwe na furaha kutoka kwa wadau mbalimbali jijini humo ambao watashiriki katika ufunguzi huo.
Aidha, Msama alitoa wito kwa wakazi wa jiji la Mwanza na Kanda ya Ziwa kujitokeza kwa wingi kufanikisha ufunguzi wa duka hilo ambalo ni mkombozi wa wizi wa kazi za sanaa, hasa nyimbo za Injili Tanzania.
“Kwa kuwa nawajali wananchi, naomba wajitokeze kwa wingi kujipatia kazi halisi na kuondokana na wizi wanaofanyiwa na wachache wasioitakia mema tasnia ya sanaa hapa nchini,” amesema Msama.
Aliongeza kuwa huo ni mwanzo wa maendeleo ya kudhibiti kazi za sanaa, baada ya Mwanza anatarajia kupanua wigo kwa kufungua maduka katika mikoa mingine.
CHANZO FULL SHANGWE

No comments:
Post a Comment