Nyota wa Ivory Coast Gervinho akishangilia bao lake na Didier Drogba.
MAGOLI mawili ya vichwa ya Wilfried Bony na Gervinho yaliyopishana kwa sekundi 98 yameipa ushindi wa kwanza Ivory Coast kwenye mchezo wa kundi la C wa kombe la dunia na kuilaza Japan mabao 2-1 mjini Recife.
Bony aliifungia Ivory Coast bao la kusawazisha katika dakika ya 64 na Gervinho akaongeza bao la ushindi mnamo dakika ya 66.
Japan walikuwa wa kwanza kuandika bao katika dakika ya 16 ya kipindi cha kwanza kupitia kwa nyota wao Keisuke Honda, na baada ya hapo Ivory Coast waliendelea kupoteza nafasi za kufunga.
Kutokana na uzembe huo wa washambuliaji wa Ivory Coast ilionekana ndoto ya kufuzu hatua ya 16 kutoka kundi C inaweza kupotea kutokana na ushindi waliopata Colombia dhidi ya Ugiriki katika kundi lao la C.
Tembo hao kutoka pwani ya magharibi mwa Afrika walimuacha nahodha wao , Didier Drogba katika kikosi kilichoanza ambapo aliingia katika dakika ya 62 akichukua nafasi ya Die na alifanya vizuri kwa dakika hizo alizocheza.
Gervinho na Wilfried Bony walifunga mabao mawili ndani ya dakika mbili na kuwapa ushindi Ivory Coast.
Kusoma zaidi na kutazama picha za mechi hii bofya www.bkmtata.blogspot.com.
CHANZO FULL SHANGWE
No comments:
Post a Comment