Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday, 15 June 2014

MAMA SALMA KIKWETE MGENI RASMI KWENYE MAADHIMISHO YA SIKU YA WACHANGIAJI DAMU SALAMA KITAIFA ILIYOFANYIKA KIGOMA.

IMG_0078Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimshuhudia Ndugu Mariam Juma,42, mkazi wa Shirika Mnarani huko Kigoma akitolewa damu wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku ya waqchangiaji damu iliyofanyika kitaifa huko Kigoma tarehe 14.6.2014. Katikati ni Ndugu Franco Mwikwa, Afisa mtoa damu salama kutoka ofisi ya Kanda ya Magharibi yenye makao yake makuu mjini Tabora.IMG_0082Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimshuhudia Ndugu Mariam Juma,42, mkazi wa Shirika Mnarani huko Kigoma akitolewa damu wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku ya waqchangiaji damu iliyofanyika kitaifa huko Kigoma tarehe 14.6.2014. Katikati ni Ndugu Franco Mwikwa, Afisa mtoa damu salama kutoka ofisi ya Kanda ya Magharibi yenye makao yake makuu mjini Tabora.IMG_0104Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapungia mamia ya wananchi wa mji wa Kigoma waliokuwa kwenye maandamano ya kuadhimisha kilele cha siku ya wachangiaji damu salama zilizofanyika kitaifa mjini hapo tarehe 14.6.2014. Wengine katika picha ni (kulia kwenda kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya, Naibu Waziri wa Afya Dkt. Kebwe Stephen Kebwe, Mheshimiwa Margareth Sitta, Mbunge na Mwisho ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma Ndugu Walid Kabourou.IMG_0129Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapungia mamia ya wananchi wa mji wa Kigoma waliokuwa kwenye maandamano ya kuadhimisha kilele cha siku ya wachangiaji damu salamaIMG_0131Baadhi ya wananchi wa Kigoma wakipita kwa furaha mbele ya mgeni wa heshima wakati wa maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu duniani iliyoadhimishwa kitaifa huko Kigoma ambapo Mama Salma alikuwa Mgeni rasmi.IMG_0152Baadhi ya wananchi wa Kigoma wakipita kwa furaha mbele ya mgeni wa heshima wakati wa maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu duniani iliyoadhimishwa kitaifa huko Kigoma ambapo Mama Salma alikuwa Mgeni rasmi.IMG_0196Wacheza ngoma kutoka wilaya ya Makamba nchini Burundi walioalikwa kwenye maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu salama wakicheza ngoma ya utamaduni  kwa umahiri mkubwa.IMG_0250Mgeni Rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu salama kitaifa Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi wa Mkoa wa Kigoma kwenye uwanja wa Lake Tanganyika taehe 14.6.2014.IMG_0276Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizindua rasmi mfumo wa Kuhifadhi kumbukumbu za wachangiaji damu Tanzania  (Blood Establishment Computer system-BSCF) wakati wa Maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu salama duniani kwenye sherehe zilizofanyika kitaifa huko Kigoma tarehe 14.6.2014.IMG_0298Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi tuzo Ndugu Emmanuel Essay, Mfanyakazi wa KCMC inayotolewa na Mpango wa Taifa wa Damu salama kwa mwanaume aliyechangia damu kuliko wote hapa nchini kwa mwaka 2013/14. Ndugu Essay ametoa damu mara 53 katika kipindi hicho.IMG_0303Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa tuzo kwa Ndugu Restituta Mushi  kwa kuwa mwanamke aliyechangia kutoa damu salama kuliko wanawake wote hapa nchini katika mwaka2013/14. Restituta anatoka katika Mkoa wa Mwanza na ameweza kutoa damu mara 28 katika kipindi hicho.IMG_0383Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki kupiga ngoma na kucheza pamoja na wananchi waliokuwa wakiwaburudisha wananchi wa Kigoma waliohudhuria maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu salama iliyofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Lake Tanganyika tarehe 14.6.2014.
IMG_0388Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki kupiga ngoma na kucheza pamoja na wananchi waliokuwa wakiwaburudisha wananchi wa Kigoma waliohudhuria maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu salama iliyofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Lake Tanganyika tarehe 14.6.2014.
 PICHA NA JOHN  LUKUWI
CHANZO FULL SHANGWE

No comments:

Post a Comment