Wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi wa Wilaya ya Ilala wakipata maelezo jinsi ya kurekodi utabiri wa kila siku katika studio ya TMA iliyopo katika ofisi za Mamlaka- Makao Makuu, Ubungo Plaza.
Meneja wa ofisi ya utabiri Bw. Samwel Mbuya akitoa maelezo jinsi mchakato wa uandaaji utabiri unavyofanyika wakati wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi wa Wilaya ya Ilala walipotembelea ofisi hizo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Dkt. Agnes Kijazi ( wa pili kulia waliokaa) akifuatiwa na mwakilishi wa mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Wilaya ya Ilala Bi. Angelina Malembeka katika picha ya pamoja na wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi na uongozi wa TMA.
Jumuiya ya Wazazi (CCM) Wilaya ya Ilala imetembelea
ofisi za Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini ili kujifunza shughuli mbali mbali zinazofanywa
na Mamlaka ikiwemo utayarishaji wa
utabiri na usambazaji wake husasan taarifa za hali mbaya ya hewa.
Katika msimu
wa MASIKA uliomalizika mwezi Mei mwaka
huu maeneo mengi ya Wilaya ya Ilala yaliathirika na mvua kubwa zilizokuwa
zikinyesha katika maeneo mengi nchini.
Aidha wajumbe wa Jumuiya waliipongeza
TMA kwa kufanikisha kutoa tahadhari kwa wakati hivyo kupunguza madhara ya vifo
kwa wananchi waishio maeneo hatarishi na kuahidi kushirikiana na Mamlaka katika
kusambaza taarifa za hali ya hewa kwa wananchi wote hasa wa Jiji la Dar es
Salaam.
Jumuiya ya Wazazi wa Wilaya ya Ilala iliongozwa na Bi Angelina Malembeka (Diwani wa Msongola)
aliyemuwakilisha Mwenyekiti wa Jumuiya, Katibu wake Lugano Mwafonga, diwani
wa Kariakoo Abdulkarim S. Masamaki , wenyeviti na makatibu kata wa Wilaya
ya ilala ambapo ujumbe huu ulipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi na menejimenti yake.



.jpg)
No comments:
Post a Comment