WALIOKUWA mabingwa watetezi wa kombe la dunia, Hispania wamekamilisha ratiba ya kundi lao la B kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Australia.
Mabao ya Hispania yamefungwa na David Villa, Fernando Torres na Juan Mata.
Ushindi huo angalau umewafariji Hispania ambao sasa wanaondoka kwenya michuano ya mkwa huu ya kombe la dunia nchini Brazil wakiwa na pointi 3 kibindoni.
Katika kikosi cha leo, nahodha na kipa mkongwe wa Hispania, Iker Casillas alikaa benchi na kushuhida Reina akicheza dakika zote tisini.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com
CHANZO FULL SHANGWE
No comments:
Post a Comment