WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
TAARIFA
YA UFUATILIAJI WA UGONJWA WA HOMA YA DENGUE
1.
UTANGULIZI
Mnamo
tarehe 27 Januari 2014, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilipata taarifa za
kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa homa ya dengue katika Kliniki ya
‘International School of Tanganyika’ iliyopo Manispaa ya Kinondoni katika jiji
la Dar es Salaam. Taarifa hiyo ya awali ilionyesha kuwepo kwa jumla ya wagonjwa
6 katika kituo hicho bila vifo.
Aidha,
mlipuko wa ugonjwa huu si mpya hapa nchini kwani uligundulika kwa mara ya
kwanza mnamo Juni 2010 mkoani Dar es salaam ambapo idadi ya watu 40
walithibitika kuwa na
2.
UGONJWA WA HOMA YA DENGUE
Homa
ya dengue ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi ambacho kinaenezwa na mbu wa aina
ya Aedes. Dalili za ugonjwa huu ni homa ya ghafla,mwili kuchoka, kuumwa
na viungo, kuvimba tezi na kupatwa na harara. Uwepo wa homa, kuumwa kichwa maumivu ya viungo na uchovu ndio dalili kuu
za ugonjwa huu. Dalili hizi huanza kujitokeza kuanzia kati siku ya 3 na
14 tangu mtu alipoambukiwa kirusi cha homa ya dengue. Kwa wakati mwingine
dalili za ugonjwa
huu zinaweza kufanana sana na dalili za malaria. Kuna aina 3 tofauti za namna
ugonjwa huu unavyoweza kujitokeza iwapo mtu aking`atwa na mbu mwenye virusi
hivi;
i. Homa ya dengue (Dengue Febrile
Illness):
Aina hii huambatana na dalili kuu tatu za homa kali ya ghafla, kuumwa
kichwa na maumivu ya viungo au uchovu. Asilimia kubwa ya watu hapa nchini
waliothirika wamekuwa na aina hii ya dalili.
ii. Dengue ya damu (Dengue
Haemorrhagic Fever):
Aina hii ya homa ya dengue huambatana na dalili za mgonjwa kutokwa na
damu kwenye fizi au puani, vile vile kutokwa na damu chini ya ngozi.
Iwapo mgonjwa huyu ataumia sehemu yoyote ni rahisi kwake kupoteza damu nyingi
kupitia kwenye michubuko.
iii. Dengue ya kupoteza fahamu
(Dengue Shock syndrome): Aina hii ya homa ya dengue huambatana na mgonjwa
kupoteza damu nyingi ambayo hupelekea mgonjwa kupoteza fahamu.
Aina
ya pili na ya tatu ni aina zenye dalili mbaya ambazo zinaweza kuhatarisha
maisha ya mgonjwa na hatimaye kusababisha kifo. Kwa Tanzania, hadi sasa ni aina
ya kwanza ya Homa ya Dengue imeripotiwa.
Virusi
vya homa ya dengue vinaenezwa kwa binadamu baada ya kuumwa na mbu aina
ya “Aedes”. Mbu hawa hupendelea
kuzaliana kwenye maji yaliyotuama karibu na makazi ya watu au hata ndani ya
nyumba. Viluwiluwi vya mbu hawa huweza kuishi katika mazingara ya ndani ya
nyumba mpaka wakawa mbu kamili na kuanza kusambaza ugonjwa huu kwa binadamu.
Ugonjwa
huu hauenezwi moja kwa moja kutoka binadamu mmoja kwenda kwa mwingine bali kwa
kupitia mbu aliyeambukizwa na virusi vya homa ya dengue anapomuuma
binadamu. Homa ya dengue inaweza kutibika kama mgonjwa atapelekwa hospitali
mapema na kupatiwa matibabu ya haraka. Hakuna tiba maalum ya kutibu virusi vya denge
wala chanjo bali mgonjwa anatibiwa kutokana na dalili
zitakazoambatana na ugonjwa huu kama vile homa, kupungukiwa maji au damu.
Jinsi
ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya dengue:
o Kuangamiza mazalio ya mbu
ü Fukia
madimbwi ya maji yaliyotuama au nyunyuzia dawa ya kuua viluwiluwi
vya mbu kwenye madimbwi hayo
ü Ondoa
vitu vyote vinavyoweza kuweka mazalio ya mbu kama vile, vifuu vya nazi, makopo,
magurudumu ya magari yaliyotupwa hovyo, nk.
ü Fyeka
vichaka vilivyo karibu na makazi ya watu
ü Hakikisha
maua yandayopandwa kwenye makopo au ndoo yaharuhusu maji kutuma
ü Funika
mashimo ya maji taka kwa mfuniko imara
ü Safisha
gata za paa la nyumba ili kutoruhusu maji kutuama
o Kujikinga na kuumwa na mbu
ü Tumia
dawa za kufukuza mbu “mosquito repellants”
ü Vaa
nguo ndefu
ü Tumia
vyandarua vilivyosindikwa viuatilifu (hasa kwa wale wanalala majira ya mchana)
ü Weka
wavu kwenye madirisha na milango ya nyumba za kuishi
2.
HALI HALISI YA SASA YA UGONJWA NCHINI
11.1 Idadi ya Wagonjwa:
Kuanzia
tarehe 27 Januari hadi tarehe 6 April 2014, jumla ya wagonjwa 399 (Kinondoni – 322, Ilala – 61
na Temeke – 16)
wamethibitishwa kuwa na ugonjwa homa ya dengue. kati yao, wagonjwa
wawili (2) wamepoteza maisha;
(i) Mwanamke, umri miaka 22,
aliyefariki katika Hospitali ya Mwananyamala tarehe 14.3.2014.
(ii) Mwanamke, umri miaka 37,
muuguzi, aliyekuwa mfanyakazi wa Hospitali ya Temeke ambaye alifia hospitali ya
MNH
11.2 Maeneo yaliyoathirika
Ugonjwa
huu umeripotiwa katika kila eneo la Dar es salaam lakini Kata zilizoathirika
zaidi kwa kuwa na wagonjwa wengi zaidi ni kama zifuatatazo;
KATA
|
IDADI
|
Msasani
|
93
|
Masaki
|
68
|
Magomeni
|
54
|
Kinondoni
A/B/Manyanya
|
29
|
Mikocheni
|
21
|
Buguruni
|
20
|
Tandale
|
15
|
Sinza/Kijitonyama
|
13
|
11.3 Dalili za kuu
zilizojitokeza
Wagonjwa
wote 399 waliothibitishwa kuwa na ugonjwa walikuwa na na homa kali.. Aidha
82% ya wagonjwa walionyesha pia dalli ya kuumwa kichwa. Dalili nyingine ni
zilizojitokeza ni pamoja na kutapika, maumivu wakati wa kutoa haja ndogo,
na kuumwa tumbo.
11.4 Jinsia na Umri
Kati
ya Wagonjwa 376, 214 (54%) walikuwa wanaume na 185(46%) walikuwa ni wanawake.
Idadi kubwa ya wagonjwa waliothibitika kuwa na ugonjwa huu wako katika Umri
zaidi ya miaka 16 yaani asilimia 92. Aidha watoto chini ya umri wa miaka
5 walikuwa ni asilimia 2 tu.
1.1 Mwenendo wa Ugonjwa
Mlipuko
huu wa tatu wa dengue hapa nchini ulianza tarehe 2 Januari 2014. Ongezeko kubwa
la wagonjwa limejitokeza katika mwezi wa tatu (3) mwishoni na kushika kasi
mwezi wa Aprili, 2014 ambapo wagonjwa wengi wameongezeka.
Jedwali
No 1: Mwenendo wa Ugonjwa wa Dengue kuanzia utokee,2 Januari 2014- 6 May
2014 (N=399)
2.
HATUA ZINAZOCHUKULIWA NA WIZARA
2.1 Hatua za Muda mfupi
ü WAUJ
imetoa tamko la Serikali kwa wananchi kwa nyakati tofauti kuhusu mlipuko
wa ugonjwa wa Dengue. Tamko la kwanza lilitolewa kwenye vyombo vya habari
tarehe 04 Februari 2014 na Machi 2014. Aidha, uelimishaji kwa wananchi
unaendelea kupitia Radio, TV na magazeti. Aidha matumizi ya Vipaza sauti katika
ngazi za chini utaanza na kusimamiwa na Halmashauri za Wilaya mkoani Dar es
salaam.
ü Kuendelea
kutoa taarifa ya tahadhari ya ugonjwa huu kupitia kwa Waganga Wakuu wote wa
Mikoa na Wilaya kwa Tanzania Bara. Aidha taarifa hii pia inajumuisha namna
mgonjwa anavyoweza kutambuliwa (Ainisho la Ugonjwa), “Ukweli Kuhusu
Ugonjwa“(Fact sheet) na mwongozo wa uchukuaji wa sampuli na
matibabu.
ü Kuendelea
kutoa elimu kwa Watumishi wa afya madaktari pamoja na wanaofanya maabara kuhusu
namna ya kutambua ugonjwa huu. Aidha watumishi wa hospitali za Muhimbili,
Mwananyamala, Amana na Temeke wamekwisha kupewa mafunzo haya na bado
yanaendelea kutolewa kupitia mikutano ya kila asubuhi ya kiltaaluma
(Clinical meetings). Halmashauri zinaendelea pia kuyatoa mafunzo haya katika
ngazi za chini.
ü Kufuatilia
kwa karibu ongezeko la wagonjwa wenye homa isiyo kuwa ya malaria kwa Mikoa na
Wilaya zote nchini ili kuweza kufanya uchunguzi wa kina iwapo kuna ugonjwa huu.
ü Kuanzishwa
kwa vituo maalum vya ufuatiliaji wa ugonjwa huu katika Hospitali za Manispaa za
jiji la Dar es Salaam (Mwananyamala, Amana na Temeke Hospitali), aidha, Kituo
cha ‘ International School of Tanganyika – IST’ kilichopo Manispaa ya Kinondoni
pia kinaendelea na ufuatiliaji wa ugonjwa huu pamoja na Kituo cha Hospital ya
Muhimbili.
ü Kuimarisha
uwezo wa kutambua ugonjwa huu kwa kina kupitia maabara ya Taifa (NHLQATC)
ambapo mpaka sasa kumethibitishwa kuwepo kwa aina 2 za virusi hivi yaani DENV2
na DENV3. Vile vile Wizara imepeleka kiasi kidogo cha vipimo vya awali yaani
“Dengue Rapid Test Kits” kwa baadhi ya vituo vya Dar es salaam kuimarisha
utambuzi na vituo hivo ni pamoja na Muhimbili, Amana hospital, Mwananyamala
hospitali, Temeke Hospital, na IST kliniki.
ü Kuimarisha
ufuatiliaji wa ugonjwa huu katika vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na
mipakani kupitia mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa (saveilensi) ya IDSR .
Aidha, Wizara imetoa maelekezo kwa Waganga wakuu wa mikoa na wilaya kutoa
taarifa za wagonjwa wa Dengue Fever kupitia taarifa za kila wiki (Infectious
disease week ending).
ü Kutoa
miongozo ya ufuatiliaji wa ugonjwa huu katika maeneo ya mipakani kuhusu kutokuwepo kwa aina yoyote ya
vikwazo vitakavyowekwa kwa ajili kwa wasafiri. Aidha maelekezo hayo yameainisha
kuwa iwapo msafiri anayeondoka au kurudi nchini akiwa na dalili tajwa atoe
taarifa kwa watumishi wa afya wa mpakani ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa.
ü Kudhibiti
mbu kwa kupulizia dawa ( Fogging) katika baadhi ya maeneo yaliyoathirika katika
mkoa wa Dar es salaam. Aidha mpango wa WAUJ ni kufikia maeneo mengi zaidi
pamoja na kufanya kuweka dawa ya kuua viliwi luwi (Larviciding)” kwa
viluwiluwi.
ü Kupeleka
taarifa ya mlipuko huu Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) kama mwongozo wa
Kimataifa uvyaoelekeza.
ü Kupitia
Timu ya Taifa ya Maafa, Wizara imeandaa mpango kazi na mkakati wa muda
mfupi wa namna ambavyo ugonjwa huu utadhibitiwa ukishirikisha wadau mbalimbali.
Kimabatanisho namba 1 kinafafanua kazi zilizoaninishwa.
3.2
Hatua za muda mrefu
ü WAUJ
imeandaa Mpango Mkakati (2014 – 2018) wa kukabiliana na magonjwa ya ‘Viral
Haemerrhagic Fevers’ ikihusisha na ugonjwa wa homa ya dengue.
ü Halmashauri
za mkoa kutengeneza “strategic plan” ya kwao kwa kuangalia “prototype plan” ya
WAUJ
4.
Changamoto
4.1 Kutokuwepo na vitendanishi
vya kutosha kuanisha ugonjwa huu kwa ngazi za chini (Rapid Diagnostic kits).
Hii inapelekea ufuatiliaji wa ugonjwa huu kuwa mgumu kwa watumishi wa vituo vya
afya na kulazimu sampuli zipelekwe Maabara kuu ya Taifa -- NHLQATC.
4.2 Kutokuwepo na mpango
mkakati shirikishi wa pamoja na wadau mbalimbali wa namna ya kukabiliana na
ugonjwa huu. Aidha Wizara imeitisha mkutano wa pamoja na wadau ili kuweza
kushirikiana nao. Mkutano huu umefanyika 7.5.2014 ambao umeainisha hatua za
kuchukuliwa.
4.3 Upungufu wa wataalum
waliobobea katika kukabiliana na wadudu wadhurifu “Entomologists” katika ngazi
ya mbalimbali. Na hii inapelekea uratibu wa kazi za “vector ” kutoratibiwa
katika kiwango stahiki.
4.4 Kutokuwepo na fedha za
kutekeleza mikakati mbalimbali ya “Integrated Vector control activities” pamoja
na kukabiliana na milipuko kwa ujumla kutoka ngazi ya Taifa mpaka chini.
4.5 Jamii kutokukuelewa kuhusu
ugonjwa huu na hii ni kwa sababu ugonjwa huu bado ni mpya nchini Tanzania.
Kupitia mpango mkakati unaoandaliwa na Wizara, ushirikishwaji wa wadau wengine
zaidi ya wa afya utaanishwa ili kuweza kuandaa vielemishi na kutafuta njia
nyingine za kufikisha ujumbe.
Kiambatanisho namba 1,
MAAZIMIO
YA KIKAO CHA TIMU YA TAIFA YA MAAFA KUHUSUIANA NA DENGUE FEVER
TAREHE
7.5.2014
Kazi
|
Shughuli
|
Mhusika
|
Muda
wa Utekelezaji
|
Uratibu
wa shughuli za Dengue Kitaifa
|
Kuwasilisha
mpango kazi ulioandaliwa kwa ngazi za juu ili pia uweze kuwasilishwa Ofisi ya
Waziri Mkuu
|
WAUJ:
Epidemiolojia
|
Mara
moja
|
Uratibu
wa shughuli za Dengue mkoani Dar es salaam
|
Kuandaa
mpango mkakati wa namna ya kukabiliana na Dengue kwa kutumia prototype plan
ya mpango mkakati wa Kitaifa
|
Halmashauri
3 za Ilala, Kinondoni na Temeke
|
Tarehe
12.5.2014
|
Udhibiti
wa Mbu na viluwiluwi
|
Kuua mazalio ya mbu yaani viluwili
(Larvidicing) kwa kutumia bio-larvicide –ambao iko kwa kiasi iliyokuwa
inatumika katika mradi wa Bio larvicide kati ya Cuba na WAUJ kupitia NMCP.
Aidha kutakuwa na ushirikishwaji wa serikali za mitaa na CORPS
Kuendelea
na kufanya fogging (kuua mbu wapevu) wenye tayari vimelea kutumia viautilifu
vya kuua mbu katika maeneo yaliyotoka idadi ya wagonjwa wengi. Aidha
kutakuwa na ushirikishwaji wa serikali za mitaa na CORPS
|
Halmashauri
3 za Ilala, Kinondoni na Temeke
|
Mara
moja (Angalizo: utategemea pia hali ya hewa na mvua)
|
Usafi
wa mazingira:
Maafisa Afya wote wa Halmashauri watahusika katika kusimamia na
kuhamasisha usafi wa mazingira kwa kutumia sheria ndogo ndogo ilizojiwekea
ikiwemo na kutoa faini
|
WAUJ: Kitengo cha Usafi wa Mazingira
Halmashauri
3 za Ilala, Kinondoni na Temeke
|
Mara
moja
|
|
Maafisa
Afya ikiwemo wa kata wataelemisha wananchi namna ya kudhibiti
ugonjwa kwa vipaza sauti, uongozi wa mitaa, kugawa vielemishi. Na
vilevile kuendelea kutumia vyombo vya habari na TV
|
WAUJ: Kitengo cha Usafi cha mazingira na
Elimu ya Afya
Halmashauri
3 za Ilala, Kinondoni na Temeke
|
||
Elimu
kwa watumishi wa Afya
|
Kutoa
elimu kupitia clinical meetings katika hospitali zote za wilaya na pia
kupitia APHTA
|
WAUJ: Epidemiolojia
Halmashauri
3 za Ilala, Kinondoni na Temeke
|
Mara
moja
|
Kuimarisha
utambuzi wa ugonjwa
|
WAUJ kuwasiliana na MSD kuhusu upatikanaji
wa “Dengue Rapid Kits” ili Halmashauri ziweze kufuata utaratibu wa manunuzi
Halmashauri na pia MNH kupanga katika
mipango yao fedha za kununua kits hizi
Kwa
kipindi hiki ambapo “kits” zinaonekana kupungua katika maeneo tajwa yaani
MNH, na Hospital za Wilaya mkoani Dar es salaam, NHLQATC itatumika kupima
vipimo hivi ili kuwepo na mwenendelezo wa “Sentinel Surveillance”
|
WAUJ: Epidemiolojia na Diagnostic
Halmashauri
3 za Ilala, Kinondoni na Temeke
|
Mara
moja
|
Kuimarisha
ufuatiliaji wa ugonjwa
|
Kutengeneza
protocol ya Surveillance pamoja na alogarithm ya matibabu
|
WAUJ:
Epidemiolojia na Diagnostic
|
10.5.2014
|
Kuweka
“messages” katika Point of Entry
|
WAUJ:
Kitengo cha Afya ya Mazingira
|
Mara
moja
|
|
Ushirikishwaji
wa wadau mbalimbali katika kukabiliana na ugonjwa huu
|
WAUJ kuandika barua kwa RAS Dar es saalam
kuanisha maeneo ya utekelezaji ambao yako chini ya mamlaka yake
WAUJ
kuandika barua ya kuomba zaidi msaada wa “Dengue Rapid Kits” WHO, CDC
na USAID
|
WAUJ: Epidemiolojia na Diagnostic
WAUJ:
Epidemiolojia na Diagnostic
|
Mara
moja
|
UNICEF
kusaidia na IEC materials yaani Posters na leaflets ambazo tayari
zimeshatengenezwa
|
WAUJ:
Kitengo cha ELimu ya Afya kwa Umma
|
Mara
moja maana tayari kuna mawasiliano
|
|
WHO
kusaidia katika uelimishaji kwa kupitia kifungu cha fedha za “World Health
Day” iliyolenga masuala ya “vector”
|
WAUJ:
Kitengo cha ELimu ya Afya kwa Umma
|
Utekelezaji
unategemea barua kuandikwa kutoka WAUJ kwenda WHO
|
Imeandaliwa na:
Kitengo
cha Epidemiolojia na Ufuatiliaji wa Magonjwa
No comments:
Post a Comment