Pages

Pages

Pages

Tuesday 20 May 2014

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AANZA ZIARA MKOA WA SINGIDA

1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto na Mbunge wa jimbo la Manyoni Magharibi Mh. Paul Lwanji wakinyanyua bati juu kuwapatia mafundi  wanaojenga madarasa katika shule ya sekondari ya Mgandu wakishiriki ujenzi wa shule hiyo wakati Katibu mkuu huyo alipokagua ujenzi wa madarasa katika shule hiyo ikiwa  ni ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali kwa pamoja na wananchi, Abdulrahman Kinana yuko katika ziara ya mikoa ya Singida, Tabora na Manyara ambapo leo amewasili katika mkoa wa Singida baada ya kumaliza  ziara yake katika mkoa wa Tabora akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-ITIGI-SINGIDA)2Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifukia mti mara baada ya kupanda mti katika shule ya sekondari ya Mgandu leo.4Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akipanda mti katika  shule ya sekondari ya Mgandu.6Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akipiga kifaa cha mziki wa ala wenye asili ya watu makabila ya mkoa wa Singida.7Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua bwawa la umwagiliani katika kijiji cha Igala Itigi mkoani9 Singida8Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mhandisi wa wilaya ya Manyoni Bw. Deus Magoma wakati akielezea kuhusu mradi wa bwawa la la kilimo cha umwagiliaji katika kijiji hicho.9Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi wakati alipowasili katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Relini mjini Itigi mkoani Singida leo.10Baadhi ya wana CCM waliohudhuria katika mkutano huo.12Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mh. Mgana Msindai akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Itigia mkoani  Singida.11Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.13Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara.

CHANZO FULL SHANGWE

No comments:

Post a Comment