Rished Bade
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Rished BADE kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amemteua Bwana Rished BADE kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA).
Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Ombeni Sefue, uteulzi huu umaanza tarehe 06 Mei, 2014. Bwana BADE
anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Harry KITILYA ambaye alistaafu
tarehe 14 Desemba,2013.
Kabla ya uteuzi huo,
Bwana BADE alikuwa Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania tangu
Septemba,2012 na baadaye kukaimu nafasi ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania tangia Bwana Kitilya alipostaafu.
Kabla
ya kujiunga na Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bwana Rished BADE amewahi
kufanya kazi katika maeneo mbalimbali yaliyompa ujuzi na weledi mkubwa
kwenye mambo ya fedha na mapato kama ifuatavyo:-
Oktoba, 1995 – Mei, 2000 – Mkaguzi wa Benki za Biashara, Benki Kuu ya Tanzania.
Juni, 2000 – Juni, 2001 – Credit Manager, Akiba Commercial Bank.
Juni, 2001 – Septemba,2001 – Chief Financial Officer, Akiba Banking Corporation.
Septemba, 2001 – Machi, 2006 – Chief Operating Oficer, Barclays Bank (Uganda).
Januari, 2007 – Desemba, 2009 – Chief Executive Officer, Barclays Bank (Tanzania)
Desemba, 2009 – 2012 – Chief Financial Officer, (East and West Africa Cluster) Barclays Bank Plc Emerging Markets.
Novemba, 2010 – Septemba, 2012 – Chief Executive Officer, Tanzania Mortgage Refinance Company.
Bwana
Rished BADE ana Shahada ya Kwanza ya Bachelor of Commerce and
Management ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1995); Shahada ya Master of
Commerce in Banking and Finance ya Chuo Kikuu cha Sydney (1999), na ni
Certified Public Accountant (CPA).
Katika
kumteua kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mheshimiwa
Rais ana imani kubwa kwa elimu, uzoefu na weledi alionao, Bwana Rished
Bade kwa kushirikiana na watumishi wenzake, atatoa mchango mkubwa kwa
Taifa kwa kuzidi kuimarisha Mamlaka hiyo na kuboresha utendaji wake na
hivyo kuongeza mapato ya Serikali kwa faida ya Taifa.
“Mwisho”
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu - Dar es Salaam.
08 Mei, 2014
No comments:
Post a Comment