Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 18 May 2014

DC AELEZA MIKAKATI YA MAFANIKIO YA JIJI LA ARUSHA


Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Arusha.

MKUU wa wilaya ya Arusha , John Mongela amesema kuwa halmashauri ya jiji la Arusha limefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kutekeleza miradi yake mbalimbali kwa kipindi cha mwaka 2005 hadi 2012.
Aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mafanikio mbalimbali waliyofikia kwa kipindi hicho pamoja na changamoto ambazo zinawakabili.
Mongela alisema kuwa, kwa kipindi cha mwaka 2005 walikuwa na  jumla ya wanafunzi 46,588 katika shule za msingi  ambapo kwa sasa hivi wameongezeka hadi kufikia wanafunzi 55,697.
Aliongeza kuwa, kwa kipindi cha mwaka 2005 walikuwa na jumla ya shule za sekondari 3,776 ambapo hadi sasa  wana jumla ya shule za sekondari 22,971 sawa na ongezeko za shule za sekondari 19,000 .
Mongela akizungumzia kwa upande wa shughuli za kijami alisema kuwa, wamewezesha zaidi ya vikundi 142 vya kijamii kupata mikopo na huduma mbalimbali ambapo zaidi ya fedha taslimu milioni 50 zilitolewa kwa ajili ya kuwapatia mikopo vikundi hivyo.
Alifafanua zaidi kuwa, katika kuhakikisha wameboresha jiji la Arusha wamefanikiwa pia kuanzisha mradi mkubwa katika dampo la manispaa lililopo Muriet ambapo litawezesha idadi kubwa ya vijana kupata ajira kupitia mradi huo ambao tayari umeshaanza kutekelezwa.
"Unajua sisi kwa kipindi cha mwaka 2005 hadi sasa hivi tumeweza kwa kiasi kikubwa sana kuleta mafanikio katika jiji la Arusha ikiwemo afya, shulre, barabara za kati kati ya miji pamoja na huduma mbalimbali za kijamii , hivyo ni jambo la kujivunia sana kuwa tumepiga hatua kubwa na ya kuigwa na watu wote," alisema Mongela.
Akizungumzia swala la mipango miji alisema kuwa , wameweza kuhamasisha wananchi katika upimaji wa maeneo yao ikiwa ni pamoja na kupatiwa hati miliki hali ambayo itawezesha wananchi kujenga kwa mpangilio katika maeneo yao na kuondokana na msongamano mkubwa ambayo ni changamoto inayolikabili jiji la Arusha.

No comments:

Post a Comment