Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 21 May 2014

‘BADO SACCOS HAZIJAWASAIDIA WAJASIRIAMALI’


Waziri wa Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza.PICHA|MAKTABA 

Dar es Salaam. Ongezeko la idadi ya Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (Saccos), limedaiwa kutokuwa na msaada mkubwa kwa wajasiriamali wadogo.
Kauli hiyo imekuja huku serikali kupitia Waziri wa Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza ikisema vyama hivyo vimeongezeka kutoka 5,424 Machi 2012 hadi 5,559 Machi 2013.
Kwa upande wa wanachama wameongezeka kutoka 917,889 hadi 1,153,248 katika kipindi hicho, huku wakiongeza hisa, akiba na amana kutoka sh236.8 bilioni mpaka kufikia sh463.5 bilioni.
Hata hivyo, mtaalamu wa uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Humphrey Moshi, alisema pamoja na ongezeko hilo, huduma za Saccos hazijawafikia wajasiliamali wengi.
Mbali na hilo, aliongeza kuwa huduma hiyo imekuwa ikitolewa katika mfumo usiyokuwa rasmi, hivyo wajasiriamali wameendelea kukandamizwa na ukubwa wa riba za mikopo pamoja na masharti magumu yasiyokuwa na lengo la kuwasaidia.
“Mahitaji ya wajasiriamali yanaongezeka kila wakati, mikopo wanayopata ni kidogo sana, riba zao ni kubwa na masharti ni kikwazo. Kwa hivyo ili kuwasaidia wajasiliamali ni lazima saccos hizo ziunganishwe na mkondo wa benki kubwa zilizopo kwenye mfumo rasmi zinazotambuliwa” alisema.
 CHANZO MWANANCHI

No comments:

Post a Comment