Susuluka Imani Paul akiwa hospitalini.
SUSULUKA Imani Paul, kijana mwenye umri wa miaka 18, ambaye Novemba mwaka jana alikutana na unyama wa aina yake, baada ya kutafunwa sehemu kubwa ya uso wake maeneo ya mdomoni, analia kutokana na mateso makubwa yanayotokana na maumivu ya mwili pamoja na ukosefu wa fedha za matibabu na mahitaji.
Susuluka, mkazi wa Kijiji cha Nyabibuye Kakongo, wilayani Kibondo mkoani Kigoma, alijeruhiwa vibaya kwa kutafunwa usoni na baba yake mzazi, Imani Paulo (36) kwa kung’atwa kisha kunyofolewa macho, pua na meno kubaki nje.
Inadhaniwa
kuwa wakati wa tukio hilo, baba yake mzazi alikuwa hana akili za
kawaida na inadaiwa kuwa hadi sasa bado anashikiliwa na polisi huku
uchunguzi zaidi wa tukio hilo ukifanywa.
Kwa sasa, kijana huyo ambaye anadai kuishi katika mazingira magumu kutokana na kukosa kwake fedha za kujikimu, yupo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akitibiwa.
“Nateseka
sana, inaniuma sana, baba yangu mzazi alinitafuna uso mzima, kwa sasa
sina cha kuniokoa katika maisha, fedha za kwenda India sina japo
serikali imeahidi kunipeleka, lakini natakiwa kuwa na fedha za kujikimu
kama shilingi milioni 1.8, hizo zitasaidia kupata vibali vya kusafiria
na mahitaji binafsi, naomba Watanzania waokoe maisha yangu,” alisema
Sululuka ambaye anatarajiwa kupelekwa India na serikali hivi karibuni.
Awali
taarifa za kijana huyu zilieleza kuwa alikuwa ametafunwa na mwajiri
wake lakini sasa ameamua kufunguka kwa madai kuwa aliogopa baba yake
angekamatwa na polisi.
Kama umeguswa na kilio cha kijana huyu wa Kitanzania, mchangie ulichonacho na Mungu atakupa baraka zake na ili aweze kujikimu na hata kumsaidia kwa matibabu kwa namba zifuatazo. Tigopesa 0653715400 na M-Pesa 0768454656.
<GPL>
SUSULUKA Imani Paul, kijana mwenye umri wa miaka 18, ambaye Novemba mwaka jana alikutana na unyama wa aina yake, baada ya kutafunwa sehemu kubwa ya uso wake maeneo ya mdomoni, analia kutokana na mateso makubwa yanayotokana na maumivu ya mwili pamoja na ukosefu wa fedha za matibabu na mahitaji.
Susuluka, mkazi wa Kijiji cha Nyabibuye Kakongo, wilayani Kibondo mkoani Kigoma, alijeruhiwa vibaya kwa kutafunwa usoni na baba yake mzazi, Imani Paulo (36) kwa kung’atwa kisha kunyofolewa macho, pua na meno kubaki nje.
Kwa sasa, kijana huyo ambaye anadai kuishi katika mazingira magumu kutokana na kukosa kwake fedha za kujikimu, yupo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akitibiwa.
Kama umeguswa na kilio cha kijana huyu wa Kitanzania, mchangie ulichonacho na Mungu atakupa baraka zake na ili aweze kujikimu na hata kumsaidia kwa matibabu kwa namba zifuatazo. Tigopesa 0653715400 na M-Pesa 0768454656.
<GPL>
No comments:
Post a Comment