Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Saturday, 23 April 2016
REMOVAL OF NON-TARIFF BARRIERS ON EAST AFRICA MAIN TRANSPORT CORRIDORS REDUCES TIME TO TRADE
EAC Elimination of NTB Act cited as landmark milestone supporting the progressive elimination of NTBs within the EAC. NTB Act a first in Africa
April 21st, 2016, Nairobi: A recently conducted independent evaluation of the Non-Tariff Barrier (NTB) to trade programs in East Africa indicate that removal of key NTB’s have contributed to a 14 per cent reduction in time taken to import goods from each East African country. Further, it has contributed to a 20 per cent reduction in time taken to export goods from each EAC country (from 33 days to 26 days).
MPANGO WA KUSAIDIA KAYA MASIKINI (PSSN) WABADILISHA MAISHA YA WANANCHI VIKUGE, KIBAHA
Mkurugenzi Mkazi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA), Natalia Kanem (kulia) akifanya manunuzi ya bidhaa zinazotengenezwa na wanakijiji wa Vikuge ambao wamewezeshwa na mpango wa PSSN wa TASAF. (Picha na Modewjiblog)
Washirika wa maendeleo nchini wametembelea vijiji viwili Vikuge na Mwanabwito vilivyopo Wilayani Kibaha kwa ajili ya kutazama miradi ya kusaidia kaya masikini ambayo imeanzishwa kwa msaada wa fedha ambazo zinatolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ambapo washirika hao wamekuwa wakitoa fedha ili kusaidia miradi hiyo.
LIGI YA MABINGWA WA MIKOA KUANZA MEI 14, 2016
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetangaza Mei 14, 2016 kuwa tarehe ya kuanza kwa Ligi ya Mabingwa wa mikoa (RCL) itakayozishirkisha bingwa wa kila mkoa kutoka katika mikoa 27 nchini.
SDL LIGI NDOGO KUANZA MEI 11
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuanza kwa ligi ndogo Mei 11, 2016 katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam itakayozishirikisha jumla ya timu nne.
BAADA YA KASHFA YA RUSHWA, TFF YAIPANDISHA MBAO FC LIGI KUU YA VIDACOM
African Lyon
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeitangaza klabu ya Mbao FC ya jijini Mwanza kupanda Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao kutoka katika kundi C ya Ligi Daraja la Kwanza chini (StarTimes League).
TFF imeitangaza Mbao FC kfuatia maamuzi ya Kamati ya Nidhamu ya TFF yaliyotolewa April, 2016 ya kuzishusha daraja timu nne kutoka kundi C baada ya kukutwa na hatia ya upangaji matokeo.
Saturday, 16 April 2016
MWANAFUNZI MTANZANIA ASHIRIKI ONYESHO LA UBUNIFU IKULU YA MAREKANI
Stephen Mwingira na Wendy Ni, wakiangalia kwa makini jinsi Rais Obama anavyoelekezwa namna ya kutumia simu kuendesha mashine hiyo katika Onyesho la ubunifu wa kisayansi ambalo lilifadhiliwa na Rais Barack Obama katika Ikulu ya Rais ( White House Science Fair 2016)
April 13, 2016, Rais wa Marekani, Barack Obama, alifadhili onyesho la mwisho katika utawala wake, onyesho lililohusu ubunifu katika Nyanja za sayansi ambalo limewahusisha wanafunzi kuanzia shule za awali, msingi hadi za sekondari kutoka States mbalimbali za Marekani.
Kwa miaka sita tangu mwaka 2010, Kiongozi huyo wa Marekani amekuwa akifadhili onyesho hilo lijulikanalo kama White House Science Fair ambalo limekuwa likifanyia katika Ikulu yake (White House) lengo likiwa ni kuhamasisha wanafunzi kupenda masomo ya sayansi, hisabati, teknolojia na ufundi ( STEM)na hivyo kuibua vipaji vya ubunifu m iongoni mwa wanafunzi ( young inventors).
Katika onyesho hilo la Aprili 13 jumla ya wanafunzi 130 walishiriki baada ya kukidhi vigezo vya kuingia katika onyesho hilo. Miongoni mwa wanafunzi waliopata fursa hiyo adhimu ya kushiriki baada ya kukidhi vigezo ya ubunifu wao ni mwanafunzi mtanzania Stephen Wilfred Mwingira ambaye pamoja na wenzake wawili Armo Halwah na Wendy Ni wanaosoma Baruch College Campus High School ya jijini New York, wamebuni kifaa cha gharama nafuu (vacuum cleaner) kinachoweza kutumika katika kusafisha njia za reli za chini ya ardhi ( Subways).
Stephen Mwingira na timu yake, walipata fursa ya kuelezea na kuonyesha mbele ya Rais Obama namna gani kifaa walichobuni ( Vacuum Cleaner) kinavyoweza kufanya usafi kwa kufungwa kwenye treni na hivyo kusaidia katika kuzifanya njia za treni ( subways) kuwa katika mazingira ya usafi na hivyo kupunguza gharama za usafishaji.
Katika miaka sita tangu Rais Obama ambaye yeye binafsi amejipambanua kama mpenzi na shabiki mkubwa wa sayansi na ubunifu, onyesho hilo limekuwa motisha na kivutio kikubwa kwa walimu, wanafunzi, wafadhili na wataalamu waliobeba katika masuala ya sayansi, teknolojia na hesabu.
Kila mwaka State dining room ya Ikulu hugeuzwa kuwa eneo la maonyesho ambapo wanafunzi hujipanga na kuonesha vifaa walivyobuni au kutoa maelezo ya kisayansi ya namna ya kutatua tatizo Fulani kwa kutumia teknolojia nafuu.
Katika kutambua mchango wa Rais Barack Obama katika kuwahamasisha wanafunzi kupenda masomo ya sayansi, Ikulu ya White House imetangaza kwamba Kampuni ya Oracle inayojihusisha na masuala ya teknolojia ya Komputa katika miezi kumi na nane ijayo itawekeza dola za kimarekani 200 milioni kwaajili ya masomo ya sayansi ya computa kwa wanafunzi wa kimarekani.
Katika maelezo yake kwa vyombo vya habari kabla na baada ya kuhitikishwa kwa onyesho lake la mwisho, Rais Barack Obama amesema, mara zote ambazo ameshiriki kujionea ubunifu wa vijana hao wadogo na wenye kiu na ari ya kuibua mambo mapya, amekuwa akijifunza kitu kipya na mara zote amejiona kama anayepungukiwa na kitu kutokana kile anachojifunza kutoka kwa wanafunzi hao.
“Nimeweza kujionea ubunifu wa hali ya juu, kiu, na hamu ya watoto na vijana wetu wataalamu wa kesho wa taifa letu la marekani. Ipo siku huko mbeleni nitajivunia pale ambapo miongoni mwa vijana wetu hawa watakapoweza kubuni tiba ya kansa.
Nitaangalia nyuma kwa fahari kubwa kwamba niliwawezesha vijana hawa kuibua vipaji vyao ”. Akasema Rais Obama kwa furaha huku akiwashukuru wale wote ambao kwa miaka sita mfululizo wamewezesha kwa namna moja ama nyingine kufanyika kwa onyesho hilo.
Chanzo: Michuzi Blog
RAIS MAGUFULI AZINDUA MRADI WA BARABARA YA JUU TAZARA
Rais Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) pamoja na Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida (kushoto) wakiweka jiwe la msingi kama ishara ya kuzindua rasmi Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Flyover -Tazara huku wakishuhudiwa na viongozi mbalimbali wa serikali.
TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MZFA
Shirkisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetuma salamu za rambirambi kwa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Mwanza (MZFA), kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu wa MZFA na makamu mwenyekiti wa FAT Silvanus Makalu Ngofilo aliyefariki dunia juzi jijini Mwanza.
RC DAR ES SALAAM NA KOREA KUSINI WAWEKA JIWE LA MSINGI LA HOSPITALI YA CHANIKA MANISPAA YA ILALA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia) na Makamu wa Rais wa Shirika la Koica la nchini Korea Kusini, Taemyon Kwon, wakiweka tofali kwa pamoja kuashiria uweka wa jiwe la msingi la Hospitali ya Chanika iliyopo Manispaa ya Ilala, inayojengwa kwa ufadhili wa nchi hiyo Dar es Salaam jana. Ujenzi huo hadi kukamilika utagharimu Sh. bilioni 8.8 za Kitanzania.
LIGI KUU KUENDELEA WIKIENDI
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo minne kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini, huku kila timu ikisaka ushindi katika michezo hiyo ili kujiweka katika mazingira mazuri kwenye msimamo wa ligi.
MALINZI AMPONGEZA RAVIA
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amempongeza Ravia Idarous Faina wa kuchaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) katika uchaguzi ulifanyika jana katika ukumbi wa Uwanja wa Gombani, Pemba.
SIMBA KUSHIRIKI KOMBE LA NILE BASIN
Klabu ya Simba SC ya jijini Dar es salaam imethibitisha kushiriki michuano ya Kombe la Nile Basin Club Championship, inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) itakayoanza kutumia vumbi Mei 22, 2016 nchini Sudan.
RAIS WA SUDANI KUSINI SALVA KIIR AWASILI NCHINI NA KUTIA SAINI MKATABA WA KUJIUNGA RASMI NA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akipokea maua kutoka kwa
mtoto Sharon Innocencia Shiyo mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Ikulu
jijini Dar es Salaam na kulakiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano
Dkt. John Pombe Magufuli.
Friday, 15 April 2016
HEART MARATHON KUFANYIKA APRILI 26
Mratibu wa Heart Marathon Dkt. Omary Chillo (katikati)
akiongea na waandishi wa habari kuhusu
mashindano ya mbio maalum za kupambana na ongezeko la magonjwa
yasiyoambukiza zijulikanazo kama Heart Marathoni zinazotarajiwa kufanyika
Aprili 26 mwaka huu jijini Dar es salaam, kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Heart Marathon
Dkt. Chaka Halfani na kulia kwake ni Kaimu Katibu Chama cha Riadha
Tanzania Bi. Ombeni Zavala.
UKATILI WA KIJINSIA SOKO LA TEMEKE STEREO JIJINI DAR ES SALAAM BADO KUNA CHANGAMOTO KUBWA
Katibu wa Soko la Temeke AStereo, Omary Seif Mangilile akizungumza katika kapmpeni ya kuongeza uelewa dhidi ya ukatili wa kijinsia masokoni iliyofanyika katika soko la Temeke Stereo Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia ni Meneja wa Mradi huo wa kupinga ukatili huo, Grace Mateh kutoka Shirika la Equality for Growth (EfG). Hata hivyo katika soko hilo bado kunachangamoto kubwa ya vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia hasa kwenye eneo la wauza mihogo kama ilivyoelezwa na baadhi ya wafanyabiashara katika soko hilo.
TAMISEMI MKOANI MWANZA YAONGOZA KWA RUSHWA
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rusha Mkoani Mwanza (Pichani) Mhandisi Ernest Makale, leo ametoa taarifa ya Utendaji kazi wa taasisi hiyo mbele ya Wanahabari katika kipindi cha robo mwaka (Januari hadi Machi) mwaka huu.
BENKI YA NMB NA MFUKO WA MCF WASAINI MKATABA KUZIKOPESHA HOSPITALI BINAFSI
Subscribe to:
Posts (Atom)












