Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday, 26 June 2015

UNESCO KUWAWEZESHA WAJASIRIAMALI JAMII YA KIMASAI NGORONGORO


Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues  (kulia) akimwelezea Katibu Tawala, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Lemuel Kristian Kileo (wa pili  kushoto), namna mradi wa ujenzi wa kituo cha sanaa ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya ujasiliamali wa  bidhaa zinazotokana na mifugo kwa akinamama na wasichana kutoka Kata tano za Wilaya ya Ngorongoro  utakavyotekelezwa juzi katika Kijiji cha Ololosokwan. Wengine ni maofisa miradi kutoka UNESCO wakishuhudia. Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akimwelezea Katibu Tawala, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Lemuel Kristian Kileo (wa pili kushoto), namna mradi wa ujenzi wa kituo cha sanaa ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya ujasiliamali wa bidhaa zinazotokana na mifugo kwa akinamama na wasichana kutoka Kata tano za Wilaya ya Ngorongoro utakavyotekelezwa juzi katika Kijiji cha Ololosokwan. Wengine ni maofisa miradi kutoka UNESCO wakishuhudia.

WAPATIKANA SIKU TANO BAADA YA AJALI YA NDEGE


Mama mmoja amepatikana hai pamoja na mwanawe siku tano baada ya ndege walimokuwa wakisafiria kuanguka mwituni huko Colombia.

BURUNDI KUENDELEA NA RATIBA YA UCHAGUZI KAMA KAWAIDA

Gervais Rufyikiri aliyekuwa makamu wa rais wa Burundi amekimbilia Ubelgiji.
Serikali ya Burundi imesema haitashiriki katika mazungumzo yaliyodhaminiwa na Umoja wa Mataifa yakilenga kupunguza hali ya uhasama uliopo kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wenye utata.

UMOJA WA ULAYA KUWAPA HIFADHI WAHAMIAJI HARAMU

Boti yenye wakimbizi kutoka Tunisia ikiwasili kisiwa cha Lampedusa nchini Italia
Viongozi wa Umoja wa Ulaya wakiendelea na kikao chao hadi usiku wa manane mjini Brussels wamekubaliana kuwahamisha maelfu ya wahamiaji ambao waliingia katika nchi za Italia na Ugiriki.

ALIOA SIKU TATU TU KABLA YA KUFARIKI DUNIA


Kijana mmoja barubaru alimuoa mpenzi wake siku tatu tu kabla yake kuaga dunia kutokana na Saratani ya damu lukaemia.

AL SHABAAB YASHAMBULIA KITUO CHA AMISOM


Takriban watu 30 wamepoteza maisha yao baada ya shambulizi la kigaidi katika kituo cha kijeshi cha wanajeshi wa kimatifa wa kulinda amani nchini Somalia Amisom.

WAISLAMU WAMCHINJA MTU MMOJA UFARANSA, WAJERUHI MWINGINE


Mtu mmoja amechinjwa na mwengine akajeruhiwa vibaya baada ya shambulizi la kiislamu katika mji wa Lyon Ufaransa.

Wednesday, 24 June 2015

WANAHABARI WASHINDANA KUTAMBUA LADHA ZA BIA ZA TBL DAR

 Meneja uzalishaji wa TBL, Bw. Charles Nkondola akikabidhi zawadi ya bia aina ya Kilimanjaro Twist kwa mshindi wa tatu wa kutambua aina ya ladha ya Bia za  Kampuni ya Bia Tanzania (TB)L, Aloyce Ndeileko wa This Day, iliyofantika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

BALAA: MWALIMU MKUU ASHIRIKI NGONO NA WANAFUNZI WA MIAKA 13!

Mwalimu Mkuu Anne Lakey
Mwalimu mmoja mkuu amekiri kufanya ngono na wavulana wawili wenye umri mdogo.

MTUNZI WA FILAMU YA TITANIC, JOHN HORNER AFARIKI DUNIA

John Horner
James Horner, mtunzi nguli wa eneo maarufu kwa watu maarufu la Hollywood ambaye aliandika na kushinda katika tuzo za Oscar juu ya filamu maarufu ulimwenguni ya Titanic,amefariki dunia mjini California kutokana na ajali ya ndege akiwa na umri wa miaka 61.

Tuesday, 23 June 2015

PAGAN AMUM AREJESHWA SERIKALINI SUDAN KUSINI

Pagan Amum
Katibu mkuu wa chama tawala nchini Sudan kusini amerudishwa katika wadhifa wake baada ya kuishi kwa mwaka uhamsihoni nchini Kenya.

BUHARI ASEMA ZAMA ZA UFISADI ZIMEKWISHA

Rais Mohammadu Buhari akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry
Rais mpya nchini Nigeria Muhammadu Buhari amewaambia magavana kuwa siku za matumizi mabaya ya fedha zimekwisha.

PATA UNDANI WA KARENZI KARAKE, JASUSI WA RWANDA ALIYEDAKWA UINGEREZA

Luteni Jenerali Karenzi Karake
Nchini Rwanda anajulikana zaidi kwa jina fupi KK. Alivyokamatwa ,luteni jenerali Karenzi Karake, mwenye umri wa miaka 54 ni mtu wa kwanza wa ngazi ya juu kutoka kwa orodha ya watu 40 walio na wadhfa mkubwa katika jeshi la RPF orodha iliyotolewa na jaji mmoja wa Uhispania akitaka wakamatwe.

SOKO LA GIKOMBA LATEKETEA KENYA


Soko kubwa la kuuza nguo kukuu nchini Kenya la Gikomba katika mji wa Nairobi limeteketea.

RAIS KIKWETE AMTUNUKU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, MBARAK ABDULWAKIL NISHANI YA UTUMISHI MREFU NA MAADILI MEMA DARAJA LA KWANZA

Displaying PIX 1..JPG
Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akimvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, wakati wa sherehe ya kutunuku Nishani iliyofanyika kwenye Ukumbi mpya wa Mikutano Ikulu, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

NTIMIZI AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO VYA MILIONI 40

Mussa Ntimizi
Na Hastin Liumba, Uyui
MWENYEKITI wa chama cha mpira wilaya ya Uyui mkoani Tabora Musa Ntimizi amemwaga vifaa vya michezo katika wilaya ya Uyui vyenye thamani ya Shs. milioni 40.

WANAOVALIA SURUALI ZA KUBANA KUKIONA


Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 35 alilazimika kutolewa ndani ya suruali ndefu aina ya Jeans, baada ya miguu yake kuvimba kupita kiasi.

P. DIDDY AKAMATWA KWA SHAMBULIO

P. Diddy
Mwanamuziki mashuhuri wa nyimbo za Hip hop P Diddy amekamatwa kwa kushukiwa kumshambulia mtu kwa silaha mjini Los Angeles.

RWANDA YASHUTUMU KUKAMATWA KWA OFISA WAKE

Karenzi Karake
Rwanda imeshutumu uamuzi wa mamlaka za Uingereza kumkamata kiongozi wake wa ujasusi wa Rwanda, Karenzi Karake, ambaye anatakiwa Uhispania kwa madai ya uhalifu wa kivita.

JOTO KALI LAUA WATU 700 PAKISTAN


Waziri mkuu nchini Pakistan Nawaz Sharrif ametaka hatua za dharura kuchukuliwa huku idadi ya watu waliofariki kutokana na wimbi la joto katika mkoa wa kusini wa Sindh ikifikia 700.