






Sehemu ya kiwanda cha kuzalisha vinywaji baridi jamii ya Cocacola ,kiwanda cha Bonite Ltd mjini Moshi.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Kanda ya Kaskazini
ZAIDI ya wateja 15,000 wa vinywaji baridi vinavyozalishwa na
kampuni ya Bonite Bottlers Ltd ya mjini Moshi
wamejishindia zawadi mbalimbali kupitia promosheni ya “Coke Studio kunywa na
Ushinde “ inayoendelea .
Wateja hao wamejishindia zawadi baada ya kununua soda jamii
ya Cocacola ,Fanta na Sprite zikiwa
katika ujazo wa mililita 350 na mililita 500 huku wengine 22 wakikabidhiziwa
zawadi zao za Televisheni za kisasa za ukubwa wa inchi 32.
Hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao kutoka mikoa ya
,Arusha,Kilimanjaro na Manyara imefanyika katika viunga vya Kiwanda cha Bonite
Bottlers Ltd na baadae washindi wote walipata nafasi ya kutembelea na kujionea
uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za Bonite.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao Meneja
Mauzo wa kampuni ya Bonite Bottlers Ltd ,Boniface Mwase alisema wateja wa
bidhaa zinazozalishwa na Bonite kila mmoja yupo kwenye nafasi ya kujishindia
zawadi kwa kutumia kiasi cha Sh 500 na sh 1000.
“Zawadi ambazo tumezitoa leo (Jana) ni televisheni 22 kwa washindi ambao
wamejitokeza ,zipo zawadi za soda za bure ,zipo zawadi za fedha kiasi cha sh
5000 hadi 10,000,hizi zinatolewa pamoja hapo mteja anapokunywa soda anashinda
papo hapo “alisema Mwase.
Alisema kumekuwa na hamasa kubwa kwenye shindano la Coke
Studio kunywa na ushinde na washindi wameendelea kupatikana kutoka maeneo yote ambayo bidhaa
za Bonite zinapatikana na kwamba kila
atakayeshinda atafikishiwa zawadi yake kwa wakati.
Mwase alisema Bonite
imekuwa na utaratibu wa kufanya Promosheni kila mara lengo likiwa ni kurejesha
seheu ya faida inayopata kwa wateja ambao wamekuwa wakiunga mkono kampuni hiyo
kwa kutumia bidhaa zake.
“Nitoe wito kwa wateja wetu waendelee kutumia soda za jamii
ya Coca Cola kwa sababu zawadi bado ni nyingi na kila mmoja ana nafasi ya
kushinda,”alisema Mwase.
Zainaabu Lusoke ,mkazi wa Arusha ni mmoja wa washindi wa
Televisheni katika promoshen ya Coke Studio kunywa na ushinde amesema zawadi
hiyo inatokana na Mama yake mdogo aliyemtaka kuokota kizibo alichotupa pindi
aliponunua Soda aina ya Fanta.
“Katika shindano hili sikutegemea kama nitashinda, nilinunua
soda nikatupa kile kizibo, ma mdogo akaniambia kwa nini unatupa, nikamwambia hivi vizibo vya Bonite
vimeandikwa Jaribu Tena, akaniambia kachukue kile kizibo ,ndipo nilipotizama
nikakuta nimeshinda TV,” alisema Zainabu.
Washindi waliojinyakulia zawadi za Televisheni ni pamoja na
Mariam Mkara, Saumu Rashid, Hadija Mmbughu, Emanuel Magige, Lightnes Lusega, Mwanahawa
Miraji, Mohamed Hussein na Fadhili Lyimo.
Wengine ni Hilda Silayo, Judith Assey, Haruna Mohamed, Nasibu
Juma, Happy Kombe, Fii Mkwanda, Emanuel John, Nembris Simon, Godfrey Wilson, Zainabu
Salim, Rajabu Miraji, Said Massatu na Laurant Mlingi.
No comments:
Post a Comment