Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 12 December 2016

MAJINA YA TIMU ZA TAIFA U23 YATAKIWA KUPENDEKEZWA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetoa nafasi kwa wafamilia wa soka kupendekeza majina ya timu za Taifa za vijana wenye umri wa chini ya miaka 23 za wanawake na wanaume.

Timu hizo za Taifa ya Wanawake U23 na Timu ya Taifa ya Wanaume U23, zitaingia kwenye program ya kuandaliwa kuwania nafasi ya kucheza fainali za michuano ya Olimpiki zitazayofanyika jijini Tokyo, Japan; mwaka 2020.
Wadau wa mpira wa miguu wanaombwa kupendekeza majina hayo kupitia anwani za tanfootball@tff.or.tzmjselestine@yahoo.co.uk au Namba za simu +255 678 297727, +255 624 121812, +255-22-2182032 au nukunishi (faksi) +255-22-2182031.
Tayari Tanzania ina majina ya timu za Taifa ya wanaume wakubwa (Senior National Team) ambayo ni Taifa Stars, Timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania ‘Twiga Stars’ na Timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Queens’.
Pia zimo timu ya Taifa ya Vijana ya wenye umri wa chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’; Timu ya Taifa ya wanawake wenye umri wa chini ya miaka 20 ‘The Tanzanite Queens’ na timu ya Taifa ya Vijana ya wenye umri wa chini ya mika 17 ‘Serengeti Boys’

No comments:

Post a Comment