Pages

Pages

Pages

Thursday 15 September 2016

SERIKALI ITOE TAMKO KUTEKWA KWA WATANZANIA NCHINI CONGO


TAARIFA KWA UMMA
CHAMA Cha ACT Wazalendo, kimepokea kwa mstuko taarifa ya kutekwa kwa Magari 12 ya kusafirisha Mizigo yaliyokuwa safarini nchini Congo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Chama cha wamiliki wa Malori Tanzania(TATOA) iliyomnukuu  mmoja wa wamiliki wa malori hayo Azim Dewji wa Kampuni ya Simba Logistic ,imeeleza kuwa kati ya magari hayo 12 magari manane(8) ni za kitanzania na yaliyobaki ni kutoka Kenya na kwamba gari nne za Kitanzania tayari zimechomwa moto huku madereva wakiwa wamechukuliwa na waasi.
Kwamba  tukio hilo limetokea sehemu inayoitwa Kasebebena na Matete ambayo ni kilometa 30 kutoka mji wa  Namoya huku madereva wawili wa kitanzania walioshikiliwa mateka wakifanikiwa kutoroka.
Kwa nafasi yetu ya Chama ambayo moja ya malengo makuu ni kuhakikisha watanzania wanakuwa salama popote waendapo, tunaitaka serikali ya jamhuri ya Muuungano wa Tanzania itoe taarifa rasmi juu ya tukio hili na iseme inachuka hatua gani kuhakikisha watanzania wanarudi salama
Pia tunaitaka serikali kuwahakikishia ulinzi watanzania wote walio katika nchi mbali mbali zinazokabiliwa na migogoro ya ndani kabla ya madhara makubwa hayajawakuta katika maeneo hayo.
John Patric Mbozu
Katibu Mambo ya Nje
ACT Wazalendo.
15 Septemba 2016

No comments:

Post a Comment