Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 1 September 2016

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AMWAPISHA BW. DOTO JAME KUWA KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO


Benny Mwaipaja, MoFP
Dar es salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amemwapisha Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (pichani), Ikulu, Jijini Dar es salaam, baada ya kumteua kushika wadhifa huo jana.
Baada ya kuapishwa, Katibu Mkuu huyo amekula kiapo kingine cha maadili mbele ya Kamishna wa Maadili, Jaji (Mst.) Salome Kaganda, ambaye amemtaka kutekeleza majukumu yake kwa uadilifu mkubwa ili kuisaidia nchi kufikia malengo yake ya kuwatumia wananchi katika sekta ya fedha na uchumi
Bw. Doto James anachukua nafasi ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Servacius Likwelile, ambaye Mhe. Rais Dkt. Magufuli, amesema atampangia kazi nyingine.
Doto James, ambaye kitaaluma ni mchumi, alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango akishughulikia sera, atawaongoza manaibu makatibu wakuu wengine watatu walioko katika Wizara ya Fedha na mipango.

No comments:

Post a Comment