Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo
Na
Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma
09/09/2016
Serikali
imeanza kutatua changamoto za umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara kwa kuiunganisha
mikoa hiyo kwenye umeme wa gridi ya taifa kupitia njia ya KV 400.
Akijibu
swali la Mhe. Vedasto Ngombale lililohusu kiini cha ukatikaji wa umeme leo
mjini Dodoma, Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo amesema kuwa
suala la umeme kutoka Lindi hadi Mtwara linachangamoto nyingi za kiufundi
ambapo hupelekea tatizo hilo kujitokeza.
Prof.
Muhongo amesema kuwa mitambo ya Somangafungu inachangamoto kwani umeme
unaofuliwa kutoka mitambo hiyo unatumika katika Wilaya za Kibiti, Kilwa na
Rufiji ambapo hutumia Megawati 7.5 kwa kutumia gesi asilia.
Aidha,
Serikali kupitia Shirika la Umeme la Taifa (TANESCO) imeanza ukarabati katika
Wilaya za Kibiti, Kilwa na Rufiji wa mitambo miwili yenye uwezo wa kuzalisha
umeme kwa jumla ya Megawati 5 unaotarajiwa kukamilika Novemba, 2016 na
utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 3, ambapo ufufuaji wa mtambo wenye uwezo
wa kuzalisha Megawati 2.5 unategemewa kuanza mwezi Oktoba mwaka huu.
Kwa
upande mwingine Naibu Waziri wa Nishati na Madini Medard Kalemani amesema kuwa
Serikali imeanza utekelezaji wa ujenzi wa njia ya umeme itakayounganisha Wilaya
ya Liwale na Nachingwea ambapo kwa sasa zinatumia umeme kutoka kituo cha
kuzalisha umeme kwa kutumia Gesi Asilia kilichopo Mtwara.
Naibu
Waziri huyo, amesema kuwa hatua iliyofikiwa kwa mpango huo ni ujenzi wa njia ya
umeme wa msongo wa KV 33 yenye urefu wa Kilomita 14.5 kutoka Nachingwea hadi kijiji
cha Luponda na kilomita 73 kutoka Liwale hadi kijiji cha Nangano kuelekea
Nachingwea.
Zaidi
ya hayo, TANESCO inaendelea na ukaguzi, usafirishaji na ukarabati wa
miundombinu ya kusambaza umeme kwa lengo la kuwaondolea wananchi kero ya
kukatika kwa umeme hatua ambayo itaondoa tatizo katika maeneo hayo.
No comments:
Post a Comment