Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 1 July 2016

RAIS PAUL KAGAME ASEMA, TANZANIA KUFANYA BIASHARA NA RWANDA INATUPA IMANI


Na Immaculate Makilika, MAELEZO

RAIS wa Serikali ya Rwanda Mheshimiwa Paul Kagame amesema nchi yake inapata amani kuona kuwa Tanzania iko tayari kufanya nao biashara.

Hayo yamesemwa leo, wakati Rais Kagame alipokuwa akifungua maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwl. Nyerere  vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

“Inatupa amani kuona Tanzania iko tayari kufanya biashara na Rwanda, naahidi kuwa tutaendelea kujifunza   zaidi na kufanya biashara zaidi” amesema Rais Kagame.

Rais Kagame, ameendelea kwa  kusema kuwa “ sote ni wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na nchi za Ukanda wa kati, zenye lengo moja, hivyo wananchi wetu watafaidika kwa kuwa na miundombinu itakayosadia kukuza biashara zetu”.

Aidha, amewataka washiriki wa maonesho hayo kuwa na mawazo mapya ya biashara yatakayosaidia kuona fursa  za biashara zilizopo katika soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kwa upande wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  amesema, katika bara la Afrika kumekuwepo na changamoto  nyingi za biashara  kama kutokuwa na ushirikiano baina ya nchi na nchi na kutojitangaza kibiashara.  Hivyo   kufanya kiwango cha biashara  kati ya nchi na nchi kuwa chini.

Rais Magufuli, ameongeza kuwa   kupitia soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki lenye nchi sita, na soko la Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) lenye watu zaidi ya milioni 40, iwe fursa ya watu kushirikiana na kujitangaza kibiashara.

Maonesho hayo ya 40 ya biashara ya kimataifa, yamekuwa na mafanikio kwa kuwepo na ushiriki wa nchi 30 kutoka sehemu mbalimbali duniani, ikiwa ni  zaidi ya nchi zilizoshiriki mwaka jana. Aidha, kumekuwepo na mabanda zaidi ya 650 na wajasiriamali 2000 ambao wanashiriki kwa kuonesha bidhaa mbalimbali, huku yakiwemo makampuni 15 kutoka nchini Rwanda.

No comments:

Post a Comment