Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday, 6 March 2016

SIMBA YAKWEA KILELENI, YAICHAPA MBEYA CITY 2-0!


Mfungaji wa bao la Simba, Danny Lyanga

Na brotherdanny.com
WEKUNDU wa Msimbazi, Simba, leo wamefanikiwa kukwea kileleni baada ya kufikisha pointi 48 kufuatia ushindi mzuri wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City, pambano ambalo limefanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Waliopeleka furaha Msimbazi walikuwa Ibrahim Ajibu na Danny Lyanga baada ya kufunga mabao mazuri na kuwaacha vijana wa Mbeya City wakiwa hawana la kufanya.
Katika pambano hilo lililokuwa na ushindani mkubwa, Simba walifanikiwa kupata bao la kuongoza katika dakika ya 75 lililopachikwa na Danny Lyanga kufuatia kazi nzuri ya kiungo Ibrahim Ajib ambaye aliwatoka mabeki wa Mbeya City, akampa pasi Awadhi Juma ambaye alipiga shuti kali lililopanguliwa na kipa wa Mbeya City, kabla ya Lyanga, ambaye alikuwa karibu, kuutumbukiza mpira wavuni.
Wakati City wanapambana kutafuta bao la kusawazisha, mashabiki wa Simba wakalipuka kwa furaha dakika ya 90 baada ya Ajibu kufunga bao la pili alipowatoka walinzi wa City upande wa kushoto na kufumua shuti kali lililowababatiza walinzi hao na kipa, kabla ya kuzama kimiani.
Ajib anashangilia bao hilo kwa kwenda ndani ya wavu wa lango la Mbeya City huku akipongezwa na wenzake.
Simba, ambayo imeshuka dimbani mara 21 na kuwazidi Azam na Yanga mchezo mmoja, inaombea dua mbaya wapinzani wake hao ili iendelee kukaa kileleni na hatimaye kunyakua ubingwa ambao imeukosa kwa misimu mitatu.
Mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa huku timu zikishambuliana kwa tahadhali na mpaka mapumziko hakuna aliyeruhusu wavu wake kutikiswa.
Katika mchezo wa leo, Simba iliwakilishwa na Vincent Angban, Emiry Nimubona/Hassan Kessy, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga, Juuko Murshid, Justice Majabvi, Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude, Hamis Kiiza/Awadhi Juma, Ibrahim Ajib, na Brian Majwega/Danny Lyanga.
Mbeya City: Hannington Kalyesebula, assan Mwasapili, Abubakar Shaban, Tumba Sued, Haruna Shamte, Kenny Ally, Raphael Alpha, Haruna Moshi ‘Boban’/Themi Felix, Geofrey Mlawa, Joseph Mahundi, na Ditram Nchimbi.

No comments:

Post a Comment