Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza na wajumbe (hawapo
pichani) wa Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi
katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Wapili
kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara hiyo, Marlin Komba. Kulia ni
Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Baraza
la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya
Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA), Esaka Mugasa. Katika
hotuba yake, Katibu Mkuu aliwataka watu wanaomiliki silaha nchini isivyo halali
kuzisalimisha haraka iwezekanavyo kabla ya operesheni ya kuwakamata haijaanza. Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Marlin Komba akizungumza na wajumbe (hawapo
pichani) wa Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi
katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam,
kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu ili aweze kuifungua warsha hiyo ya siku mbili.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwakilishi wa Katibu Mtendaji
wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa
Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa
Silaha Haramu (RECSA), Esaka Mugasa akizungumza na wajumbe (hawapo pichani) wa
Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi katika Ukumbi
wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Watatu kulia ni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira na wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara hiyo,
Marlin Komba. Katibu Mkuu katika hotuba yake ya ufunguzi wa warsha hiyo, aliwataka
watu wanaomiliki silaha nchini isivyo halali kuzisalimisha haraka iwezekanavyo
kabla ya operesheni ya kuwakamata haijaanza. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wapili kulia) akitoka katika
Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam mara baada
ya kufungua Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara hiyo, Marlin Komba, wapili
kushoto ni Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi-Makao Makuu, Hezron Gyimbi na kulia
ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Yusuph Ilembo. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza na wajumbe wa
Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi katika Ukumbi
wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba
yake, Katibu Mkuu aliwataka watu wanaomiliki silaha nchini isivyo halali
kuzisalimisha haraka iwezekanavyo kabla ya operesheni ya kuwakamata haijaanza. Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Sehemu ya wajumbe wa Warsha ya
Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi wakimsikiliza Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (hayupo
pichani) wakati alipokuwa akizungumza na wajumbe hao katika Ukumbi wa Bwalo la
Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam kabla ya kuwafungulia warsha
yao ya siku mbili itakayojadili umasishaji wa Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha
ya Mwaka 2015. Hata hivyo, katika hotuba yake, Katibu Mkuu aliwataka watu
wanaomiliki silaha nchini isivyo halali kuzisalimisha haraka iwezekanavyo kabla
ya operesheni ya kuwakamata haijaanza. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati waliokaa),
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara hiyo, Marlin Komba (wapili kushoto
waliokaa), Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi-Makao Makuu, Hezron Gyimbi (wapili
kulia), Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Yusuph Ilembo (kulia) na
kushoto ni Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na
Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha
Haramu (RECSA), Esaka Mugasa, wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa
Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi. Warsha hiyo
ya siku mbili ilifunguliwa na Katibu Mkuu, Rwegasira katika Ukumbi wa Bwalo la
Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO
YA SERIKALI,
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
YA NCHI
No comments:
Post a Comment