Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 10 December 2015

MAGUFULI ATAKIWA KUSHUGHULIKIA MAADILI NA MIHADARATI



Rais Dk. Magufuli

Na Mwandishi Wetu, Pemba
Rais John Magufuli ameombwa kurudisha maadili ya utumishi wa umma kwa kusimamia sheria za maadili kikamilifu ili watu wasitumie siasa kupora uchumi na rasilimaili za taifa huku wakitumia nafasi hizo kufanya biashara ya mihadarati na kujinufaisha misaamaha ya kodi kwa asilimia 100 ambayo imewatajirisha wachache huku nchi ikiendelea kuwa maskini.

Wito huo ulitolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa madhehebu ya dini nchini ambaye pia kiongozi wa Kanisa la Kipentekoste nchini, Mchungaji William Mwamalanga ambapo pia alisisitiza kuwa kuna haja ya mawaziri wote waliokuwemo kwenye utawala wa awamu ya nne kurudisha mali zote walizopora.
Mchungaji Mwamalanga alisema, kitendo cha Rais aliyeondoka Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na mwaziri wengine kuondoka kimya kimyaa bila kueleza hadharani mali walizoingia nazo na wanazotoka nazo kulingana na Sheria za Maadili ya Utumishi wa Umma kunaua kabisa maana ya sheria hiyo na kugeuka wimbo wa danganya toto ambao ulihimizwa   kwenye serikali ya awamu ya nne huku baadhi wabunge wakiitwa kwenye Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, ambapo hata ripoti zao hazijawahi kuwekwa hadharani.
Mchungaji Mwamalanga ambaye aliongoza ujumbe wa viongozi wa dini wakiwemo maaskofu na mashekhe na wanaharakati wa amani kutoka nchi za Maziwa Makuu, Afrika na Ulaya kwa lengo la kuhimiza uongozi wa haki, amani  na kupinga matumizi ya mihidarati kwa vijana, alisema uwazi katika uongozi ndiyo njia pekee itakayodumisha amani na kulinda rasilimali za nchi.
Viongozi wengine Sheikh Dk. Ahmad Mohammed, Sheikh Ogowi Ramadhani na Bishop Dk. Mical Daniel wameonya kwamba Afrika kwa sasa inakabiliwa tatizo baya la wanasiasa wengi kukimbilia kutawala badala ya kuongoza huku wakibainisha kwamba uongozi ni kuonyesha njia. Wameonya kwamba, tamaa ya kutawala inazifanya hata chaguzi nyingi barani humo kupoteza maana kutokana na wanasiasa kutumia rushwa, hila na wizi ili waingie madarakani kwa nia ya kujilimbikizia mali.
“Tunaona watu waliingia madarakani wakiwa maskini lakini wanapotoka madarakani wanakuwa matajiri kufuru huku wakiwa wamehodhi njia kuu nyingi za uchumi na kuwaachia wananchi kamkate kadogo ambako huendelea kung’ang’aniana,” wanasema.
Kuhusu rushwa pamoja na mihadarati, viongozi hao wameomba ziwepo sheria kali hata za vifo kwa wahusika kama ilivyo kwa China na kwingineko kwani ndiyo njia muhimu kulinda uchumi wa pamoja na maendeleleo ya kasi.
Wanasema mafanikio makubwa ya kupambana na rushwa na mihadarati nchini China yametokana na uwepo wa sheria kali za vifo, hivyo wamemuomba Rais Magufuli kuruhusu sheria hizo nchini Tanzania ili kutokomeza hali hiyo.
Katika hatua nyingine, viongozi hao walikutana na watu mbalimbali wakiwemo wanasiasa na jamii ya kawaida ambao wamemuombea Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein kuruhusu hofu ya Mwenyenzi Mungu kwa kuheshimu matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015 badala ya kurudia uchaguzi ambao kuna kila dalili kuwa hautakuwa huru wala haki haitasimamiwa.
Wanasema marudio ya chaguzi nyingi duniani yameleta maafaa makubwa ambapo wananchi hugonganishwa wenyewe kwa wenyewe huku walafi wa utawala wakijiongeza muda kama ilivyo nchini Burundi kwa kigezo kuwa hawawezi kuacha nchi ikiwa kwenye vurugu.

No comments:

Post a Comment