Maeneo ya Ngome ya waasi nchini Syria
Urusi imeanza kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya wanaompinga rais wa Syria Bashar al-Assad.
Mashambulizi yameripotiwa kulenga maeneo yanayodhibitiwa na waasi ya miji ya Homs na Hama na kusababisha madhara.
Marekani imesema ilipatiwa taarifa hizo saa moja kabla ya mashambulizi kutekelezwa.
Maafisa wa ulinzi wa Urusi wamesema wamekuwa wakiwalenga wanamgambo wa Islamic State, lakini maafisa wa Marekani wamesema mashambulizi hayo hayakuonekana kulenga ngome ya IS.
Marekani na washirika wake wamekuwa wakisisitiza kuwa Rais Bashar al-Assad aachie madaraka, huku Urusi imekuwa ikimuunga mkono Assad kuendelea kubaki madarakani.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesema nchi yake ilikua imejiandaa kuunga mkono hatua za kijeshi za Urusi lakini iwapo tu Operesheni zake zitakuwa dhidi ya makundi ya IS na al-Qaeda.
BBC
No comments:
Post a Comment