Rais Muhammad Buhari akihutubia kongamano la viongozi wa dunia huko New York Marekani
Rais mpya wa Nigeria Jenerali Muhammadu Buhari atahudumu pia kama waziri wa mafuta.
Msemaji wa rais Femi Adesina amethibitisha kuwa Jenerali Buhari ambaye katika miaka 80 alipoiongoza nchi hiyo alishikilia wadhfa wa waziri wa mafuta atahudumu kama waziri.
Hata hivyo naibu waziri ndiye atakayechukua majukumu ya kila siku katika wizara hiyo.
Buhari ambaye aliahidi kupambana dhidi ya rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma inayotokana na mafuta amekuwa nchini Marekani katika kikao cha viongozi wa dunia cha kongamano la umoja wa mataifa huko New York.
Uchimbaji mafuta unachangia asilimia 70% ya pato la taifa katika uchumi huo mkubwa zaidi barani Afrika hata hivyo asilimia kubwa ya pesa hizo huibiwa na kufichwa nje ya nchi.
Jenerali Buhari anatarajiwa kutangaza rasmi baraza la mawaziri wake hii leo.
Rais huyo mpya wa Nigeria alichukua hatamu za kuingoza taifa hilo yapata miezi minne iliyopita.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment