Pages

Pages

Pages

Thursday 3 September 2015

UKAWA WAMJIBU DK. SLAA, WASEMA TUHUMA ALIZOTOA ZINALIPASUA TAIFA

Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, James Mbatia

Na Emmanuel Mtengwa, Mwananchi Digital
Dar es Salaam. Siku moja baada ya Dk Willibrod Slaa kuibuka na kuelezea kilichotokea wakati wa kumkaribisha Edward Lwoassa Ukawa na hatimaye kutangaza kuachana na siasa, Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, James Mbatia amejibu tuhuma zilizotolewa na Dk Slaa huku akitahadharisha kuwa zinalenga kulipasua taifa.
Mbatia ambaye ni Mwenyekiti Taifa wa NCCR Mageuzi amesema leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza an waandishi wa habari kuwa mambo yaliyozungumzwa Dk Slaa ikiwa ni pamoja na kashfa zakuwatuhumu viongozi wa dini kuhongwa na Lowassa si yakweli na yanaweza kuligawanya taifa.

Mbatia  amesema kuwa Dk Slaa angepaswa kutoa hoja zake na sio kuwashambulia watu binafsi wakiwemo viongozi wa dini.

‘’Mimi nilitegemea Dk. Slaa ataeleza hoja zake, lakini hoja za kashfa za kuwahusisha viongozi wa dini hasa maaskofu ni hoja ambazo ni wazi zimelenga kulipasua taifa’’ alisema Mbatia.

Pia Mbatia amekiri kuwa Dk. Slaa alishiriki katika mchakato wa kumkaribisha Lowassa lakini katika vikao vyote Lowassa hakuwahi kusema atakuja na wabunge toka Chama Cha Mapinduzi.

"Katika kikao cha kujadili juu ya kumpokea Lowassa tukiwa na viongozi waandamizi wa Ukawa pamoja na Lowasaa kilichofanyika tarehe 20 mwezi wa saba , Lowassa hajawahi kutamka kuwa   atakuja na wabunge 50 toka Chama cha Mapinduzi, wala hakusema atakuja na wenyeviti wa mikoa na wilaya."

Akizungumzia suala la Dk. Slaa kudai alipewa rushwa ya Sh500m ili kuzuia ripoti ya Richmond isiingie bungeni, Mbatia ameuliza kwanini Dk.Slaa hakuripoti kipindi hicho na anakuja kuongelea sasa.

“Nashangaa tangu sakata la Richmondi litokee ni miaka saba hadi sasa, lakini Dk. Slaa hakuwahi kusikika akilizungumzia, na kwanini hakuripoti kwenye vyombo vinavyohusika," alihoji Mbatia.

Aidha Mbatia amevitaka vyombo vya habari kuandaa midahalo maalum ambayo itawahusisha viongozi wa kisiasi ili kujibu mambo wanayotuhumiwa
CREDIT: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment