Pages

Pages

Pages

Sunday 2 August 2015

WAYAHUDI WAANDAMANA DHIDI YA WANAMGAMBO

Picha ya mtoto wa Kipalestina aliyechomwa moto hadi kufa
Maelfu ya watu nchini Israeli wameshiriki kwenye maandamano wakiitaka serikali kuchukua hatua kali zaidi dhidi ya wayahudi wanaotajwa kuwa wanamgambo.
Waandamanaji katika mji wa Tel Aviv walionyesha uzalendo wao kwa familia ya mtoto Mpalestina ambaye aliuawa siku ya ijumaa wakati nyumba katika eneo la ukingo wa magharibi ilipochomwa moto na wayahudi wenye itikadi kali.
Maandamano mengine yalifanyika katika eneo kulikofanyika shambulizi siku ya alhamis ambapo watu sita walidungwa visu wakati wa mkutano wa wapenzi wa jinsia moja.
Israel
Wakati huo huo kijana Mpalestina ambaye alipigwa risasi na wanajeshi wa Israeli wakati wa maandamano ya siku ya ijumaa ameaga dunia.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment