Pages

Pages

Pages

Sunday 2 August 2015

WANAJESHI WAWILI WA UTURUKI WAUAWA KATIKA SHAMBULIO

Shambulizi Uturuki
Wanajeshi wawili wa Uturuki wameuawa kwenye shambulizi la bomu katika kituo kimoja cha kijeshi mashariki mwa nchi.
Wanajeshi wengine ishirini na wanne walijeruhiwa kwenye shambulizi hilo lililotokea katika wilaya ya Dogubayazit wakati wanamgambo waliendesha gari lililokuwa limejazwa vilipuzi na kugonja jengo moja.
Utawala umewalaumu waasi wa kikurdi wa PKK.
Jeshi la Uturuki limekuwa likiendesha mashambulizi ya angani dhidi ya PKK kaskazini mwa Iraq siku za hivi majuzi.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment