Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 20 August 2015

SBL YAPELEKA UZINDUZI WA TUZO YA UBORA WA THAMANI KWA WAKAZI WA MWANZA NA MOSHI

 Wafanyakazi wa kampuni ya Serengeti Brewieries Limited wakiwa na Mabalozi wa kinywaji hicho wakati wa  kutambulisha Tuzo ya Dhahabu ya Monde inayotambulika kimataifa baada ya bia ya Serengeti Premium Lager kukidhi viwango vya juu vya ubora katika hafla iliyofanyika katika Baa ya Oriental ,Majengo mjini Moshi mwishoni mwa wiki.

 Meneja mipango ya biashara, matukio na uhamasishaji  wote wa kampuni ya Serengeti Breweries Limited Bw. Denis Tairo akikabidhi kiasi cha Tsh 50,000 fedha taslim kwa mkazi wa Kona ya Bwiru,jijini Mwanza Bw. Godfrey Urio aliyeibuka mshindi wa shindano la “Serengeti Masta” wakati wa kusherekea uzinduzi kampeni ya tuzo ya dhahabu ya ubora wa thamani ya Monde Selection ambapo kwa mwaka huu bia ya Serengeti Premium Lager toka SBL imejinyakulia medali tatu za dhahabu kutokana na ubora wake.Hafla hiyo ambayo ilikua mahususi kwa wakazi wa kanda ya ziwa, ilifanyika katika baa ya “The dreams” iliyopo Kona ya Bwiru jijini Mwanza. Shindano hilo litafanyika Tanzania nzima na kuibua Mshindi mmoja kwa kila kanda na mwisho kumuibua wa kitaifa. Kauli mbiu ya kampeni hii ikiwa ni “TUNAIJUA BIA NA SERENGETI PREMIUM LAGER NDIO YENYEWE”.
Mkazi wa Kona ya Bwiru jijini Mwanza Bw.Godfrey Urio akicheza muziki mara baada ya kuibuka mshindi wa shindano la “Serengeti Masta” wakati wa kusherekea uzinduzi kampeni ya tuzo ya dhahabu ya ubora wa thamani ya Monde Selection ambapo kwa mwaka huu bia ya Serengeti Premium Lager toka SBL imejinyakulia medali tatu za dhahabu kutokana na ubora wake. Hafla hiyo ambayo ilikua mahususi kwa wakazi wa kanda ya ziwa, ilifanyika katika baa ya “The dreams” iliyopo Kona ya Bwiru jijini Mwanza. Shindano la “Serengeti Masta” litafanyika Tanzania nzima na kuibua Mshindi mmoja kwa kila kanda na mwisho kumuibua wa kitaifa. Kauli mbiu ya kampeni hii ikiwa ni “TUNAIJUA BIA NA SERENGETI PREMIUM LAGER NDIO YENYEWE”.

No comments:

Post a Comment