Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 21 August 2015

RAIS NKURUNZIZA AAPISHWA KWA MUHULA WA TATU BURUNDI

Rais Pierre Nkurunziza akila kiapo jana
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ameapishwa kwa muhula wa tatu uliozua utata.
Mwandishi wa BBC Prime Ndikumagenge nchini Burundi anasema kuwa sherehe hiyo imefanyika jana kwa mshangao mkubwa kwa kuwa rais Nkurunziza alitarajiwa kuapishwa wiki ijayo.
Hata hivyo hakuna kiongozi wa taifa lolote aliyehudhuria sherehe za kuapishwa kwake huku Afrika kusini ikishirikishwa na waziri mmoja kulingana na shirika AFP.
Mataifa kadhaa yakiwemo yale ya China na Urusi yalituma mabalozi wao.

Nkurunziza

Mabalozi wa Marekani na muungano wa Ulaya walisusia lakini wakashirikishwa na maafisa wa nyadhfa za chini.
Umoja wa Afrika haukutuma waangalizi.
Takriban watu 10 wameuawa tangu Nkurunziza atangaze mnamo mwezi Aprili kwamba atawania muhula wa tatu wa urais.
Serikali inaushtumu upinzani ambao unasema kuwa muhula huo ni kinyume na sheria kwa kuzua ghasia.

Nkurunziza

Umoja wa Afrika,muungano wa Ulaya na wizara ya maswala ya kigeni ya Marekani wote wameonyesha wasiwasi wao kwamba uchaguzi huo wa mwezi Julai haukuwa huru na wa haki.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment